Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Jimbo la Makambako mkoani Njombe, Deo Sanga, ametoa wito kwa mamlaka husika kuwachukulia hatua wote wanaoeneza ujumbe wa uchochezi unaoweza kuhatarisha amani ya nchi, ikiwemo kuchora vibonzo vyenye taswira ya Rais kwa lengo la kumkashifu na kumkejeli.
Akizungumza bungeni jijini Dodoma wakati wa mjadala wa taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2024, pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Sanga amesema vitendo vya aina hiyo ni hatari kwa ustawi wa taifa na vinapaswa kudhibitiwa mapema.
Mbunge huyo ameiomba wizara husika pamoja na vyombo vya dola kufuatilia kwa karibu mienendo ya namna hiyo ambayo alisema inakiuka maadili ya taifa, na inapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.