PreGE2025 Mbunge Dkt. Samizi Akabidhi Saruji Mufiko 50 na Mabati 79 Shule ya Msingi Kwizera

PreGE2025 Mbunge Dkt. Samizi Akabidhi Saruji Mufiko 50 na Mabati 79 Shule ya Msingi Kwizera

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

WhatsApp Image 2025-04-24 at 07.15.43.jpeg

Mhe. Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe tarehe 23 Aprili, 2025 amefanya ziara Kata ya Kumwambu amekabidhi Saruji mifuko 50 Shule ya Msingi Kwizera ili kukamilisha nyumba ya mwalimu

Pia, Mbunge Dkt. Florence Samizi ametoa Mabati 79 kwa ajili ya Ujenzi wa Kivuli cha wajasiliamali wadogo wadogo katika soko la Nyamkokoma Nabuhima ili wajasiliamali hao waweze kuuzia Kivulini.

Naye, WEO wa Kata ya Kumwambu, ndugu Bendiliba Y. Jumanne, ametoa shukrani za dhati kwa Mbunge Dkt. Florence Samizi kwa namna ambayo amewiwa kusaidia vifaa vya ujenzi ambavyo vilikuwa ni hitaji kubwa katika shughuli za ujenzi

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kumwambu, Ramadhani Athuman Ntarambe amesema katika umri wake wote ndani ya CCM katika Wilaya ya Kibondo hajawahi kuona/kupata Mbunge mwadilifu kama Dkt. Florence George Samizi, Mbunge aliyetekeleza miradi mingi Jimbo la Muhambwe

Mwenyekiti Ntarambe amewataka viongozi wa CCM Kata, Tawi na mashina kuhahakikisha Mbunge Dkt. Florence Samizi wanampa kura za kishindo ifikapo kwenye uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM ili aweze kupata nafasi ya kuwaletea maendeleo katika kipindi cha miaka mitano ijayo, 2025-2030.

Aidha, Mbunge Dkt. Florence Samizi akiwa Kata ya Kumwambu na Kata ya Bitare ameomba tathimini kutoka kwa viongozi wa Kata, Matawi na Mashina, kama hawajaridhishwa na uongozi wake wamuambie ili ifikapo Tarehe 28/6/2025 asichukuwe fomu, ya kuwania muhura wa pili, jambo ambalo wajumbe wamemhakikishia achukuwe fomu ili wampe muhura wa pili kuliongoza Jimbo la Muhambwe kutokana na kazi nzuri ambazo amezifanya ndani ya uongozi wake

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mwisho; Mbunge Dkt. Florence Samizi ni Mbunge ambaye amevunja rekodi ya kukubalika na mwenye ushawishi wa hali ya juu toka Jimbo hili la Muhambwe kutawaliwa na Wabunge waliomtangulia, ikumbukwe kuwa Samizi ni Mbunge toka aliposhika hatamu kuliongoza Jimbo la Muhambwe alianza kwenda kuwaona watu mbalimbali waliopo kwenye shida na raha -misibani, Makanisani, Misikitini, na mialiko mbalimbali za sherehe ikiwemo na waliolazwa Hospital.

#VIONGOZI WA CCM KATA, TAWI NA MASHINA MUHAMBWE WAPANIA KUMPA KURA ZA KISHINDO DKT. SAMIZI 2025-2030#

Imetolewa Na;
Kitengo cha habari na mawasiliano Ofisi ya Mbunge wa Muhambwe


WhatsApp Image 2025-04-24 at 07.15.45 (1).jpeg
WhatsApp Image 2025-04-24 at 07.15.43 (1).jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-04-24 at 07.15.45.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-24 at 07.15.45.jpeg
    659.1 KB · Views: 42
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Florence George Samizi ameendelea na ziara yake Jimboni ambapo Jana Jumatano Aprili 23, 2025 ilikua zamu ya Kata ya Kumwambu.

Ndani ya Kumwambu, Mbunge Samizi amekabidhi mifuko 50 ya saruji Shule ya Msingi Kwizera kwa ajili kuunga mkono ukamilishaji wa nyumba ya Mwalimu na kutoa bati 79 kwa ujenzi wa sehemu ya kufanyia biashara kwa wajasiliamali wadogo wadogo katika soko la Nyamkokoma Nabuhima ili wajasiliamali hao waweze kuuzia kivulini.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kumwambu Ramadhani Athuman Ntarambe amesema katika umri wake wote ndani ya CCM katika wilaya ya Kibondo hajawahi kuona Mbunge mwadilifu kama Dkt. Florence George Samizi na aliyepambana kuhakikisha Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inatekeleza miradi mingi ya maendeleo.

Mbunge Samizi akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake Kata ya Kumwambu na Kata ya Bitare ameweza kuwaomba viongozi na wananchi ridhaa yao ya kurudi tena baada kupitia michakato ya Chama na wananchi.

Shughuli kubwa za kusukuma maendeleo kwenye Jimbo anazozifanya Dkt. Samizi zimefanya kutengeneza kukubalika na ushawishi mkubwa sana kukubalika na mwenye ushawishi wa hali ya juu sana kwani amekua na utaratibu wa kwenda kuwaona watu mbalimbali waliopo kwenye shida na raha, misibani, makanisani, misikitini, na mialiko mbalimbali za sherehe ikiwemo na waliolazwa hospitali n.k.
 

Attachments

  • IMG-20250424-WA0023.jpg
    IMG-20250424-WA0023.jpg
    659.1 KB · Views: 35
  • IMG-20250424-WA0020.jpg
    IMG-20250424-WA0020.jpg
    532.5 KB · Views: 46
  • IMG-20250424-WA0023.jpg
    IMG-20250424-WA0023.jpg
    659.1 KB · Views: 27
  • IMG-20250424-WA0024.jpg
    IMG-20250424-WA0024.jpg
    452.7 KB · Views: 44
  • IMG-20250424-WA0028.jpg
    IMG-20250424-WA0028.jpg
    846.1 KB · Views: 36
Nguo za ccm za kazi gani katika ziara ya mbunge jimboni kwake? Alafu ilipokaribia octoba ndio tumeanza kuwaona walikuwa wapi miaka mitano iliyopita???
 
Policcm hawaoni taharuki na viashiria vya uvunjifu wa amani?Ila Kwa CDM sababu kibao kenge hawa!
 
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Florence George Samizi ameendelea na ziara yake Jimboni ambapo Jana Jumatano Aprili 23, 2025 ilikua zamu ya Kata ya Kumwambu.

Ndani ya Kumwambu, Mbunge Samizi amekabidhi mifuko 50 ya saruji Shule ya Msingi Kwizera kwa ajili kuunga mkono ukamilishaji wa nyumba ya Mwalimu na kutoa bati 79 kwa ujenzi wa sehemu ya kufanyia biashara kwa wajasiliamali wadogo wadogo katika soko la Nyamkokoma Nabuhima ili wajasiliamali hao waweze kuuzia kivulini.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kumwambu Ramadhani Athuman Ntarambe amesema katika umri wake wote ndani ya CCM katika wilaya ya Kibondo hajawahi kuona Mbunge mwadilifu kama Dkt. Florence George Samizi na aliyepambana kuhakikisha Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inatekeleza miradi mingi ya maendeleo.

Mbunge Samizi akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake Kata ya Kumwambu na Kata ya Bitare ameweza kuwaomba viongozi na wananchi ridhaa yao ya kurudi tena baada kupitia michakato ya Chama na wananchi.

Shughuli kubwa za kusukuma maendeleo kwenye Jimbo anazozifanya Dkt. Samizi zimefanya kutengeneza kukubalika na ushawishi mkubwa sana kukubalika na mwenye ushawishi wa hali ya juu sana kwani amekua na utaratibu wa kwenda kuwaona watu mbalimbali waliopo kwenye shida na raha, misibani, makanisani, misikitini, na mialiko mbalimbali za sherehe ikiwemo na waliolazwa hospitali n.k.
Uchawa tu
 
Back
Top Bottom