Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mhe. Edward Ole Lekaita amekabidhi vifaa tiba kituo cha Afya cha Engusero (Milioni 100), Zahanati ya Ngipa (Milioni 18) na Zahanati ya Nchinila (Milioni 18) vyenye thamani ya shilingi milioni 136.
Edward Ole Lekaita amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Vijana Ndorokony na kusema kuwa Serikali imeshatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa Bwawa
Mhe. Edward Ole Lekaita amesema kuwa Kata ya Njoro imepata fedha nyingi ikiwemo zaidi ya Shilingi Milioni 700 za kituo cha Afya cha Mwanya huku akichangia Mifuko 50 ya Saruji kwaajili ya Marekebisho ya baadhi ya Madarasa yaliyochakaa
Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Njoro Kijiji cha Olpopong wamemtaka Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mhe. Edward Ole Lekaita kuendelea kubaki Bungeni kwaajili ya kuleta miradi mbalimbali itakayotatua kero zinazowasumbua.