Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
Serikali imesema kuwa iko kwenye hatua za Mwisho za Tathimini juu ya kiwanda cha Chai Lupembe kinachopaswa kurejeshwa Mikononi mwa Wananchi ambapo imeelezwa kuwa baada ya Tathimini hiyo ya kina kukamilika kiwanda kitarejeshwa kwa Wananchi na hakutakuwa na Mgororo wowote huku ikielezwa kuwa Mkakati wa Serikali katika Zao la Chai hususani Jimbo la Lupembe ni kushirikisha sekta binafsi pamoja na vyama vya Ushirika ambapo lengo la Serikali ni kuviwezesha ili viweze kuitengeneza Viwanda Vidogovidogo kwaajiri ya kuongeza thamani ya zao la Chai hapa Nchini.
Serikali imetoa kauli baada ya Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mh Edwin Enosy Swalle kuhoji Bungeni juu ya nini kinachoendelea na kile kinachokwamisha kiwanda hicho kurejeshwa kwa Wananchi wa Jimbo la Lupembe huku akiihoji Serikali juu ya Mpango kabambe wa kutafta Soko la Uhakika kwa Wakulima wa Chai Lupembe kwani zao hilo ndio linatajwa kama zao kuu la kiuchumi katika Jimbo hilo.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Mh Spika Kiwanda Hiki kimefanyiwa tathimini kwa zaidi ya Mwaka Mmoja sasa na Mpaka leo bado hakija rejeshwa kwa Wananchi na Mahakama kuu ilitoa amri ofisi ya Hazina kusimamia mchakato wa tathimini na kukirejesha kiwanda hicho kwa Wananchi lakini mpaka leo Wananchi wa Lupembe hawajui nini kinaendelea Naomba kupata majibu ya Serikali"Alihoji Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mh Edwin Enosy Swalle.
"Jambo la Pili Mh Spika Wananchi wa Tarafa ya Lupembe kwa maana ya kata ya Idamba,Mfriga,Lupembe yenyewe,Matembwe na Ukalawa Wanalima sana Chai na Soko la Chai bado ni changamoto kubwa naomba kauli ya Serikali ni upi mpango kabambe wa kutafta soko la uhakika kwa Wakulima wa Chai Lupembe?"Alihoji Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mh Edwin Enosy Swalle.
MAJIBU YA SERIKALI.
"Mh Spika Mbunge wa Jimbo la Lupembe amekuwa akipigania sana zao la Chai hapa Nchini,nimhakikishie Mh Mbunge kwamba pamoja na kuchelewa kwa mchakato huu hakuna yeyote anayekwamisha sio Hazina wala bodi ya chai wala sisi Wizara ya kilimo isipokuwa tu ni utaratibu ambao unatumika katika ufanyaji tathimini wa hii kazi lakini nimhakikishie mh Mbunge kwamba tuko kwenye hatua za mwisho za tathimini na ninaamini hatutaki kufanya