Mbunge Edwin Swalle Asema Utekelezaji wa Bajeti ya Kilimo Utakuwa Faraja kwa Wakulima

Mbunge Edwin Swalle Asema Utekelezaji wa Bajeti ya Kilimo Utakuwa Faraja kwa Wakulima

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MBUNGE EDWIN SWALLE ASEMA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA KILIMO UTAKUWA FARAJA KWA WAKULIMA​

Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swalle amesema kuwa utekelezaji wa bajeti ya kilimo ukienda vyema utakuwa tiba na faraja kwa wakulima ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Bunge limeidhinisha jumla ya kiasi cha Shilingi 1,242,975,075,000 katika mwaka 2025/2026 ili kuiwezesha Wizara ya Kilimo kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ambayo inalenga kuongeza ukuaji wa Sekta ya Kilimo.

Bajeti itatekeleza vipaumbele ambavyo ni kuongeza tija na uzalishaji; kuchangia kuongeza ajira zenye staha na ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo; kuimarisha usalama wa chakula na lishe, kuimarisha upatikanaji wa masoko, mitaji na mauzo ya mazao nje ya nchi; kuimarisha maendeleo ya ushirika pamoja na kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika uendelezaji wa Sekta ya Kilimo.

#BajetiYaWakulima
#BajetiYaWakulima2025/2026
#TwenzetuShambani
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2025-05-23 at 15.26.23.mp4
    15.6 MB
Back
Top Bottom