Mbunge Elibariki Kingu alipangwa kumnanga Bishop Gwajima au ndiyo kujipendekeza?

Mbunge Elibariki Kingu alipangwa kumnanga Bishop Gwajima au ndiyo kujipendekeza?

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Huyu alikuwa anaonekana kama mmojawapo wa wabunge wasio na maana sana bungeni. Lakini kwa jana ameonekana kama vile anaanza kutumika kama game changer! Wangeongea aliyanena jana akina Nape na Janauri basi mjadala ungekuwa sio mjadala tena bali mipasho.

Huyu EK ni nani? Je uwakilishi wake kwenye jimbo la kwao Iramba Mashariki ukoje? Anatumika na Samia na Serikali yake ili kumtetea against pro-JPM au ni yeye tu kaamua kujilipua ili apate maujiko? Inaonesha kaifanya Sukuma Gang Camp kuwa kama wamemwagiwa maji. Wapi Msukuma? Wapi Lusinde?
 
Mh.Elibariki Kingu yuko sahihi.

CCM ina vijana "jeuri"....ukitukana kamwe HATUKUACHI KUKUJIBU.

HASHTAG GWAJIMA AFUKUZWE CCM
 
Kiti cha uenyekiti wa CCM bado kipo....ndicho kilichopitisha GWAJIMA aweze kugombea jimboni Kawe na wakaachwa akina Komredi Furaha Dominick.

Nazi haiwezi kushindana na jiwe.

Kamwe wanachama hatuwezi kuvumilia kumuona MWANACHAMA MWENZETU akimshambulia kwa maneno mwenyekiti wetu.

Hashtag CCM IMFUKUZE GWAJIMA
 
Umtuhumu Waziri Wa Afya na mwenyekiti wetu kuwa wamepewa fedha ili TUCHANJWE....dogo hilo?!!!!
 
Kiti cha uenyekiti wa CCM bado kipo....ndicho kilichopitisha GWAJIMA aweze kugombea jimboni Kawe na wakaachwa akina Komredi Furaha Dominick.....

Nazi haiwezi kushindana na jiwe....

Kamwe wanachama hatuwezi kuvumilia kumuona MWANACHAMA MWENZETU akimshambulia kwa maneno mwenyekiti wetu......

Hashtag CCM IMFUKUZE GWAJIMA
Chama Cha Mapinduzi kinachojiita ccm chini ya Samia Suluhu hassan hakina msuli wa kumfukuza Dkt Rashid Gwajima kwenye nafasi ya ubunge au hata kumvua uanachama. Kikijaribu kupima maji kwa ugoko kitajuta
 
Gwajima amekwenda kinyume na IMANI YA 2 YA CCM.....

"Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake"......

Amewashambulia kwa kedehi viongozi wetu wa CHAMA.....

AMEWATUHUMU KUWA WAMEPEWA FEDHA ILI WAZIPITISHE CHANJO ZA UVIKO
 
Huyu alikuwa anaonekana kama mmojawapo wa wabunge wasio na maana sana bungeni. Lakini kwa jana ameonekana kama vile anaanza kutumika kama game changer! Wangeongea aliyanena jana akina Nape na Janauri basi mjadala ungekuwa sio mjadala tena bali mipasho...
Kingu hana hekima na hana busara. Yeye kwa alivyojipambanua walipangwa na wabunge wote walioongea 99% walipangwa na walijiandaa.

Na ninakuhakikishia ikitokea mabadiliko sasa hivi ya serikali hao walioongea bungeni hao wabunge watapata tabu sana maana hiyo ni misimamo yao na si ya bunge. Ndiyo maana hata Spika alijichanganya kwa sababu walikuwa wanahukumu kitu ambacho hakipo
 
Chama Cha Mapinduzi kinachojiita ccm chini ya Samia Suluhu hassan hakina msuli wa kumfukuza Dkt Rashid Gwajima kwenye nafasi ya ubunge au hata kumvua uanachama. Kikijaribu kupima maji kwa ugoko kitajuta
Alifukuzwa Membe....CCM haikujuta.....Gwajima ana kaliba gani kumzidi Membe na Lowassa?!!!
 
Gwajima + Chadema = 2025

c2bff76c561e4c955808ebb537a47b4a.jpg
 
Siasa ni maneno.

Na maneno hayo hayako mfukoni kwa Gwajima.

Sasa aendelee KUPAYUKA aone kama Bunge halitomuongezea adhabu.

Na ya CCM bado inamsubiri.
Kingu hana hekima na hana busara. Yeye kwa alivyojipambanua walipangwa na wabunge wote walioongea 99% walipangwa na walijiandaa. Na ninakuhakikishia ikitokea mabadiliko sasa hivi ya serikali hao walioongea bungeni hao wabunge watapata tabu sana maana hiyo ni misimamo yao na si ya bunge. Ndiyo maana hata Spika alijichanganya kwa sababu walikuwa wanahukumu kitu ambacho hakipo
 
Kwa kweli jana nimeshangaa sana watu wanaongea kwa jazba na mikelele kibao ila mpaka sasa hawaja zijibu hoja za gwajiboy kuhusu chanjo ya corona.Mpaka watu jana wakasema Yesu ana mke hii yote ni kushindwa kujibu hoja kuntu za gwajiboy.
 
Alikuwa Lowassa na CHADEMA...
Alikuwa Membe na ACT......

Nini Gwajima?!!!
Swala ni kujaribu, kujaribu ni hulka ya kibinadamu. Lowassa na Membe wajibu, na Gwajiboy na yeye ana haki ya kujaribu kama akitaka.
 
Back
Top Bottom