Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
ESTHER MALLEKO AMUULIZA SWALI WAZIRI MKUU, WAZIRI MKUU ATOA MAELEKEZO KWA HALMASHAURI ZOTE NCHINI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Esther Edwin Malleko leo tarehe 29 Agosti, 2024 amemuuliza swali bungeni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye ametoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kujenga vibanda kwaajili ya kutengeneza mazingira mazuri kwa Wanawake na vijana ambao ni wajasiriamali.
"Mhe. Waziri Mkuu, Wanawake wengi wamekuwa wakijihusisha na biashara za mazao ya Kilimo kandokando ya barabara kuu za hapa nchini. Je, ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba Wanawake wanatengenezewa mazingira bora ikiwemo kuwajengea mabanda ili waweze kufanya biashara zao katika hali nzuri zaidi?" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, alipomuuliza swali bungeni, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
"Tumeshuhudia Wanawake sasa hivi wakiwa na mwamko mzuri wa kufanya shughuli za ujasiriamali na biashara kandokando ya barabara kama maeneo ya Gairo, Dumila, Mikese" - Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
"Zipo baadhi ya Halmashauri zimekuwa na maono, zimeendelea kuwasimamia wajasiriamali kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao kwa kuwajengea vibanda vya biashara kama ilivyo Dumila, Mikese. Utaratibu huu unawahamasisha wafanyabiashara kuhamasika kufanya biashara" - Mhe. Kassim Majaliwa
"Natoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini, zihakikishe zinaendelea kutambua wajasiriamali Wanawake na vijana wanaouza biashara zao kandokando ya barabara kwaajili ya wasafiri wanaosafiri ili watengenezewa mazingira mazuri ya kufanya biashara kwa kuwajengea vibanda" - Mhe. Kassim Majaliwa