Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE ESTHER MALLEKO AONGOZA WANAWAKE 300 KUJIUNGA UWT WILAYA YA MOSHI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Esther Edwin Malleko amefanya Mkutano katika Kata ya Kahe Mashariki, Moshi Vijijini kwaajili ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi na kuzipatia ufumbuzi
Katika Mkutano huo Wanawake takribani 300 wamejiunga na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwakuwa wanaridhishwa na kazi za Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Esther Malleko amewahimiza Wanawake wenye sifa kujitokeza kuwania nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji utakaofanyika Novemba 2024.
Aidha, Wanawake wa Kata ya Kahe hiyo wameahidi hawatamuangusha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kujitokeza kuwania Uongozi na kukipigia Kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi pamoja na kuendelea kulea watoto katika Maadili mema na kuwahimiza kuitunza amani ya Nchi yetu.
MAMA SAMIA MITANO TENA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Attachments
-
Screenshot 2024-09-22 at 20-25-01 Hon Esther Malleko (@esthermalleko) • Instagram photos and v...png1.1 MB · Views: 5 -
Screenshot 2024-09-22 at 20-24-31 Hon Esther Malleko (@esthermalleko) • Instagram photos and v...png1.3 MB · Views: 4 -
Screenshot 2024-09-22 at 20-25-14 Hon Esther Malleko (@esthermalleko) • Instagram photos and v...png1.2 MB · Views: 5 -
Screenshot 2024-09-22 at 20-25-50 Hon Esther Malleko (@esthermalleko) • Instagram photos and v...png1.1 MB · Views: 5 -
Screenshot 2024-09-22 at 20-26-06 Hon Esther Malleko (@esthermalleko) • Instagram photos and v...png1.1 MB · Views: 5