Mbunge Ezra Chiwelesa Aishauri Serikali Kuanzisha Taasisi ya Kusimamia Mifugo na Uvuvi

Mbunge Ezra Chiwelesa Aishauri Serikali Kuanzisha Taasisi ya Kusimamia Mifugo na Uvuvi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MHE. EZRA CHIWELESA AISHAURI SERIKALI IANZISHE TAASISI YA KUSIMAMIA MIFUGO NA UVUVI​

Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi mkoani Kagera Mhandisi Ezra Chiwelesa ameishauri serikali kuanzisha taasisi rasmi za kusimamia sekta ya mifugo pamoja na uvuvi ili kuwawezesha wafugaji na wavuvi kufikiwa kwa urahisi. Chiwelesa ametoa Ushauri huo Leo Mei 03, Mwaka huu bungeni Jijini Dodoma wakati kaichangia kwenye hotuba ya wizara ya Mifugo na uvuvi.

Amesema kuwa wafugaji na wavuvi wamekosa Chombo Cha kuwahangaikia sambamba na miradi mikubwa ambayo imekuwa ikitekelezwa na serikali kwa fedha nyingi na mwisho wa siku kuharibika kwa muda mfupi kwa kukosa usimamizi wa karibu.

Amesema kuwa kama serikali imeweza kuanzisha Wakala wa umeme vijijini REA, Wakala wa Barabara vijijini na mijiji TARURA na wakala wa Maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA basi ione namna ya kuanzishwa wakala wa mifugo pamoja na uvuvi.

Aidha ameitaka wizara ya Mifugo na uvuvi kuwalinda na kuwasema wafugaji ambao wamekuwa wakinyanyasika huku wakiwa wanachangia Pato la taifa kupitia mifugo yao.

Kuhusu kuanza utambuzi wa mifugo hasa Ng'ombe ianze na mifugo iliyopo kwenye Ranchi za taifa ILI waweze kujua idadi ya Mifugo hiyo huku akipendekeza wafugaji wasilipishwe wakati wa zoezi hilo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-03 at 16.56.39(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-03 at 16.56.39(2).jpeg
    32.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom