Mbunge Festo Sanga: Ziara ya Waziri Mkuu inaonyesha huko chini kuna Ombwe la Utumishi

Mbunge Festo Sanga: Ziara ya Waziri Mkuu inaonyesha huko chini kuna Ombwe la Utumishi

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Mbunge, Festo Sanga amesema kuwa ziara ya Waziri Mkuu inaonyesha huko chini kuna Ombwe la utumishi kwani watu wanasubiri Zoara ya Waziri Mkuu waweze kutatuliwa shida zao.

Ameeleza kuwa, watu wamegeuza kuajiriwa Serikalini ni kama kichaka, hawatafukuzwa wala kufanywa chochote hata wasipowajibika ndio maana mikwamo inakuwa mingi

"Tafsiri yake ni kwamba huku chini kwenye halmashauri na maeneo mbalimbali kwenye serikali yetu kuna ombwe la utumishi... Inatia aibu kuona Waziri Mkuu anaenda kutatua mambo ambayo yanatakiwa yatatuliwe na Mtendaji wa Kata au Mtendaji wa Kijiji.

"Kama hatutakuwa na Monitoring and Evaluation (Ufuatiliaji na Tathmini), Waziri Mkuu atapita, ataondoka, na matatizo yatabaki pale pale. Ni muhimu kila Waziri akapata majibu ya nini kimeendelea kwenye matatizo hayo ili tuweze kusaidiana."


Pia soma:DOKEZO - Ziara za Mwigulu zinaonesha Wananchi hawana imani na ma-DC, ma-RC na viongozi wengine wa chini. Kuna tatizo la uwajibikaji!
 
Back
Top Bottom