Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
"Mimi nakubali nimeomba radhi inawezekana ile kauli imewaudhi wengi, lakini mimi bado ni mtetezi wao wa kwenye matumizi na kuwasaidia kusoma vizuri kwa kuhakikisha wanafunzi wote wanalipiwa ada halafu tukawalipia matumizi (Boom) kwa hizo asilimia zilizopo," - Mwita Getere, Mbunge wa Bunda vijijini
===
Mbunge wa jimbo la Bunda Vijijini Mwita Getere amewaomba radhi wanavyuo wote ambao waliguswa na kauli yake ya kwamba wapo baadhi ya wanafunzi ambao hawatumii vizuri fedha za matumizi wanazopewa na serikali (Boom) huku wengine akiwataja kutumia fedha hizo kwenye ulevi.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 9, 2024, kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio ambapo alikuwa na haya ya kusema, ""Kimsingi mimi sijawahi kuona mwanafunzi anafukuzwa chuo kwa sababu hana boom' wanafunzi wengi wanatoka chuoni wakiwa wamekosa ada, ada ndiyo inamfanya mwanafunzi anaahirisha chuo au kuacha masomo," - Mwita Getere, Mbunge wa Bunda vijijini.
"Wale ambao walinielewa vibaya kwenye hili suala la kusema kwamba labda wanatumia vibaya hela ya boom, nilishasema tusameheane hayo nilizungumza kama mzee na mzazi, suala la matumizi mabaya huwezi kulithibitisha na sio rahisi kusema ni kweli ama sio kweli lakini kwa wale wanaotumia vizuri boom lao waendelee kufanya hivyo na wale wanaotumia vibaya waache," - Mwita Getere, Mbunge wa Bunda vijijini
Aidha akaomba radhi kwa wanavyuo, " Mimi nakubali nimeomba radhi inawezekana ile kauli imewaudhi wengi, lakini mimi bado ni mtetezi wao wa kwenye matumizi na kuwasaidia kusoma vizuri kwa kuhakikisha wanafunzi wote wanalipiwa ada halafu tukawalipia matumizi (Boom) kwa hizo asilimia zilizopo," - Mwita Getere, Mbunge wa Bunda vijijini
====
Pia soma:
Mchango wa Mbunge Getere wa "Wanachuo wasipewe boom" umemvua nguo
Mbunge Getere: Boom lifutwe, wanafunzi wanatumia kulewea