Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbunge wa Konde (ACT Wazalendo) Mohammed Said Issa ameibua mzozo Bungeni mara baada ya kusema kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiwezi kupata kura katika jimbo lake kwa sababu sera zao ni mbovu.
Mbunge Issa ameyasema hayo jioni ya tarehe 06 Februari, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Taarifa za Kamati ya Viwanda, Biashara Kilimo na Mifugo pamoja na Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi, na Usalama