Mbunge Jacqueline Kainja Achangia UWT Milioni 3.6

Mbunge Jacqueline Kainja Achangia UWT Milioni 3.6

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. JACQUELINE KAINJA ACHANGIA MILIONI 3.6 UWT MKOA WA TABORA, AZINDUA JUKWAA LA WANAWAKE

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja amechangia Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Tabora vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi 3,600,000 kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Awali inayomilikiw ana UWT Mkoa wa Tabora.

Katika ziara yake, Mhe. Kainja amechangia Viti na Maturubai kwa ajili ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Mbugani Wilaya ya Tabora. Pia, alitoa Mifuko 16 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya UWT Wilaya ya Tabora

"Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda Pamoja na Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wanatusisitiza sana UWT tuwe na Miradi ili tujisimiamie; Kwahiyo, naanza na ngazi ya Mkoa kama Mfano ili Wilaya ziweze kuiga kwenye Mkoa vivyohivyo kwenye Kata na Matawi" - Mhe. Jacqueline Kainja

Aidha, Mhe. Jacqueline Kainja amezindua Jukwa la Wanawake Kata ya Kamsekwa na kusema; "Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ya kipekee kwa kuanzisha Majukwa haya ambapo huko nyuma hayakuwepo, zingatieni taratibu na Misingi ya Jukwaa hili Mlioanzisha ili Jukwaa hili liwe kimbilio la Wanawake wote bila kujali itikadi zao".

FwgZhkvaEAAPyyS.jpg
FwgZimGaIAEFEmE.jpg
FwpOeOhX0AANEju.jpg
FwpOdcYWYAAZ12w.jpg
 
Back
Top Bottom