Mbunge Jimbo la Ulanga: Tatizo la Kompyuta na Photocopy Mashine Nitalimaliza

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Mbunge wa jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Salim Alaudin Hasham amesema atahakikisha anapambana kutatua changamoto ya vifaa vya mashuleni ili kuinua kiwango cha ufaulu wilayani humo.

Mbunge Salim ameyasema hayo wakati akigawa vifaa hivyo ambavyo aliahidi kwa shule tatu zitakazo fanya vizuri katika matokeo ya mwaka mzima atazipatia kompyuta na photocopy mashine ambapo shule zilizopata ni shule za msingi Ilonga, Ng’ongo na Kidugalo ambazo zote zimekabidhiwa vifaa hivyo vyenye thamani ya 11,400,000/=.


Aidha, Mbunge Salim amewataka walimu wakuu wa shule zote kushirikiana na wazazi kupata fedha kiasi cha 1,500,000/= na yeye atajazia kiasi kilichobaki ili kila shule ipate vifaa hivyo.

Kwa upande wa walimu wakuu waliopata vifaa hivyo wamemshukuru mbunge kwa jitihada zake na wameahidi kuhakikisha wanashirikiana kuondoa changamoto hiyo kwa shule zote wilayani humo.


Wilaya ya Ulanga ina jumla ya shule 86 shule za msingi 68 na sekondari 18 ambazo zote zinachangamoto za vifaa hivyo.
 

Attachments

  • GAIBP8bXgAALePw.jpg
    57.9 KB · Views: 1
Hivyo vifaa vyote havifikii hata kiwango cha mshahara wake wa mwezi, achilia mbali posho na pesa za mafuta.

Halafu usikute ni pesa za mfuko wa jimbo hizo.
 
Wekaga na # ya sim mzee

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…