Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. JUDITH KAPINGA - "WIZARA YA NISHATI IWAJENGEE UWEZO WAKANDARASI REA"
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Judith Salvio Kapinga aliongoza mafunzo ya Kamati ya Uongozi ya Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge katika Ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar.
Mafunzo hayo yaliyongozwa na Mhe. Judith Kapinga yalikuwa na na Mada mbili ambazo ni Maadili ya Viongozi wa Umma na Wabunge yanayoweza Kuathiriwa na Migongano ya Kimaslahi iliyotolewa na Sekretarieti ya Viongozi wa Umma pamoja na Wajibu wa Bunge la Tanzania kwenye Vita dhidi ya Rushwa iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Aidha, Baada ya hapo, Mhe. Kapinga aliongozana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo ilianza ziara yake Mkoa wa Tanga na kupokelewa na DAS Ndg. Rahel Mhando kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya.
Ziara hiyo ilianza kwa kutembelea na kukagua miradi ya REA Wilaya ya Korogwe tarehe 15 Machi 2023. Pamoja na kazi nzuri ya Wizara kamati haikuridhishwa na kasi ya usambazaji wa umeme vijijini kutokana na wakandarasi wachache wasio waaminifu.
Akiongea na waandishi wa Habari Makamu Mwenyekiti Mhe. Judith Kapinga alisema kamati imeshauri Wizara iwajengee uwezo wakandarasi wa ndani waweze kutekeleza majukumu yao.
Wakati huo huo, Mhe. Judith Kapinga amempongeza Rais wa JMT Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Miaka Miwili Madarakani yenye mafanikio kwa Taifa hasa katika Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu ya Msingi, Sekondari na Vyuo.