Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Aloyce Kwezi ameendelea na ziara yake katika jimbo na kutembelea miradi mbalimbali ambapo ameongea na wananchi wa Kata mbalimbali wa maeneo hayo.
"Ndugu zangu Wananchi wa Ukumbikakoko na Usinga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anawapenda Sana ndio maana aliwaruhusu Mawaziri 8 kuja na kuwatangazia kuishi kwenye maeneo yenu lakini Kiongozi mmoja wa Mkoa anaonekana kuanza kupinga Agizo la timu ya Mawaziri 8 kwamba Miradi isiletwe kwenu huku Huku akijua kuna Shule, Zahanati.
Rais ametupatia Mradi wa Maji wa milioni 440 na Ujenzi wa Daraja la Mto Ugala umewekwa kwenye bajeti. Nawathibitishia Niko pamoja nanyi na Tamko la Mawaziri 8 Halijafutwa" - Aloyce Kwezi
"Kero kubwa hapa ni kituo cha Afya, naahidi Katika Vituo vitatu ndani ya hii Miaka Miwili ijayo tutajenga kituo hapa, kwasasa tumejenga Zahanati mbili ya Igombe na Usimba zilizogharimu Milioni 100, Ujenzi wa Barabara tokea Katavi kupitia Ukumbisiganga, Zugimlole Kaliua, Ulyankulu mpaka Kahama, mwaka huu tunaanza na Ujenzi wa Daraja kuunganisha Kaliua na Mpanda" - Aloyce Kwezi.
"Hii Kata yenu imepokea zaidi ya Bilioni 1.2 nje ya Barabara ya Usimba - Igombe ya milioni 300; Tumejenga Madarasa 334 Kwa Jimbo la Kaliua yenye thamani ya Shilingi bilioni 6.6; Tumejenga Vituo vya Afya Usinge, Igalala na tumeanza Ukumbisiganga" - Aloyce Kwezi
Mbunge wa Jimbo la Kaliua ameendelea na Ziara yake Vijiji vya Uyumbu na Zugimlole na amechangia fedha Shilingi Milioni 5 Shule ya Msingi Kahama Ndogo na Shule Shikizi ya Iga Milioni 5.
Aidha, Wananchi wametoa Malalamiko ya Tembo kuharibu Mazao yao kitongoji cha Kapumbula kijiji cha Uyumbu na Mbunge amempigia simu Mhifadhi Mkuu wa Mto Ugalla Ndugu Melikasi ambapo Mhifadhi huyo ameahidi kuchukua hatua pindi wanyama waharibifu watakapotokea.