BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Mhe. Jesca David Kishoa (Mbunge wa Viti Maalum -Singida) Jana Jumamosi amefanya ziara ya kikazi katika kata ya Ibaga, Wilaya ya Mkalama. Ziara hiyo ni mahsusi ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuliongoza na kuliletea maendeleo Taifa letu. Mhe. Jesca Kishoa ameweza kutatua kero mbalimbali za wananchi kama ifuatavyo:
1. Kugawa Mitungi ya gesi ya kupikia Kwa kinamama wajasiriamali (Mama Lishe) 30.
2. Kugawa jezi za mpira Kwa timu 15 zinazotoka Kata ya Ibaga.
3. Ametembelea na kuchangia kiasi cha Tshs. 3,700,000/= ili kumalizia ujenzi wa zahanati ya Ibaga.
4. Ameviunga mkono vikundi 26 vya wanawake, wazee na vijana kwa kuviongezea akiba ya fedha kwenye shughuli zao.
5. Pia ametatua kero ya mgonjwa aliyepata ajali katika Kijiji Cha Ibaga na kesho mgonjwa huyo ataendelea na matibabu Hospitalini.
Aidha Mheshimiwa Mbunge amewahamasisha wananchi kudumisha mshikamano na kumuunga mkono Dkt. Samia Suluhu Hassan.