Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Mhe. Jesca David Kishoa, amepinga vikali kampeni ya NO REFORM NO ELECTION inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho kinapinga kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 hadi pale serikali itakapofanya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mhe. Kishoa ametoa kauli hiyo Aprili 5, 2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mwanga, Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida. Amesema kuwa kwa kuzingatia maandalizi na uimara wa vyombo vya ulinzi na usalama, hakuna atakayefanikiwa kuzuia uchaguzi huo kufanyika kama ulivyopangwa.
"Kwa jeshi hili tulilonalo la ulinzi na usalama, kuna mtu anaweza kuzuia uchaguzi huu? Jeshi limejipanga kikamilifu na lipo imara. Nawashukuru sana viongozi wa Jeshi la Polisi kwa maandalizi yao," amesema Kishoa.
Aidha, ameongeza kuwa ana imani kubwa kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Mkoa wa Singida, hususan Wilaya ya Mkalama, utampatia Rais Samia Suluhu Hassan kura nyingi kutokana na kazi kubwa na nzuri aliyoifanya nchini.