LGE2024 Mbunge Kiswaga: CCM Tumejipanga, Tujitokeze Kupiga Kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Jackson Kiswaga, mbunge wa jimbo la kalenga amefunga kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Nzihi kwa kusema kuwa uchaguzi wa kesho ni muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya kata hiyo.

kiswaga amewahutubia wananchi katika mkutano wa mwisho wa kampeni, huku aliwasisitizia wananchi umuhimu wa kushiriki kwa wingi kwenye uchaguzi, kuwa ni fursa ya kuhakikisha viongozi bora wa chama cha Mapinduzi wanachaguliwa ili kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali.

Kiswaga ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Nzihi kuonyesha mshikamano na kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuwachagua wagombea wa CCM, akisema kuwa chama hicho kimejizatiti kwa mikakati ya kuleta maendeleo na kuboresha huduma za jamii.

Amemaliza kuwa kupitia uongozi wa CCM, wananchi wataendelea kunufaika na miradi ya maendeleo, huduma za afya, elimu, na miundombinu inayowafaidi wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…