Kwa mfumo wa sasa wa bongo, sioni kama hiyo ni issue. At the end of the day ili mradi ana-deliver kwa kuwatumikia wananchi wake na kuleta maendeleo. Kukaa huko kijijini na kunywa nao kimpumu kila siku inaweza kuwa sio suluhisho la kuonekana ni mbunge mzuri na kuwatumikia anaowawakilisha.
Wapo wabunge ambao nawajua, hawakai ktk majimbo yao lakini wana coordinate vizuri shughuli za maendeleo ya maeneo yao, na kutatua kero za wapiga kura wao. Kumbuka siasa za bongo ni fitna na ushap wa kufuatilia mambo yako. Ukitegemea kuishi huko Kufakunoga, ambako simu ni zile za kukoroga, na ipo moja tu kwa DC, ndiyo huwe unawasiliana na wizara, idara n.k ktk kufuatilia mambo ya jimbo lako, hakuna kitakachofanyika kwa wakati.
Kujua matatizo ya wananchi wako, ktk inji yetu wala sio lazima uishi hapo jimboni.