Tetesi: Mbunge machachari kutikisa siasa za Tanzania na kumwaga manyanga kabla ya Julai 24

Tetesi: Mbunge machachari kutikisa siasa za Tanzania na kumwaga manyanga kabla ya Julai 24

Status
Not open for further replies.
Wasalaam wana jamvi!

Niendelee kuwatakia sikukuu njema ya amani na furaha miongoni mwenu!

Wana jamvi kama mtakumbuka siasa za tanzania zilitikiswa mwaka jana kama mara tatu hivi
Mara ya kwanza ilikuwa ni mtuhumiwa wa ufisadi kuhami upande mwingine..wengi hawakutegemea kama atapokelewa.

Mara ya pili ilikuwa kwa nguli wa siasa na Mzalendo Dr Slaa kumwaga manyanga chanzo ikiwa ni kupinga ujio wa mtuhumiwa wa ufisadi kwenye chama chao na hakuwa tayari kushiriki dhambi ya kumsafisha!

Tatu ilikuwa ni pale Prof Msomi na nguli wa uchumi alipo kataa kushiriki dhambi ya kumsafisha mtuhumiwa wa ufisadi na kuamua kumwaga manyanga!

Sasa kabla ya tarehe 24 nchi itatekwa tena na taharuki ya aina yake baada ya mbunge kijana na machachari kuvunja ukimya na kuamua kumwaga manyanga!
Taarifa zinasema mbunge huyo amekuwa kimya kwa kipindi kirefu sana na amekuwa akizushiwa anaumwa ili ionekane hiyo ni sababu kuu!

Hata hivyo amekuwa akipata wakati mgumu sana hasa pale anapo lazimishwa kutoa matamko ili ionekane yupo pamoja nao na amekuwa akikataa na kusema sitaki kuongea na kusema fulani aongee..

Jambo hili limekuwa likiwatesa sana watu wake ndani ya umoja wao na chama chao kwani ukimya wake umekuwa ukizua maswali mengi na wamejaribu kila mbinu za kumlazimisha aongee lakini wameshindwa!

Jambo la kumlazimisha aongee limekuwa likimkera sana na amekuwa akiwa sisitiza kuwa yeye amechagua kunyamaza wasi mlazimishe!

Kibaya zaidi kuna mpango wa kumlazimisha kuongea kwenye mkutano fulani tarehe 24 ambao bado haujawa confirmed! Lakini baada ya kupata habari kuwa amepangwa kuongea na kusema hataki na wasimlazimishe kwani umoja una watu wengi wa kuongea!

Sasa habari zilizopo ana mpango wa kuongea na ataongea kinacho muumiza kabla ya tarehe 24 na atamwaga manyanga na kuachana na ubunge kabisa na kwenda kusoma nje ya nchi....

Baada ya viongozi wake kupata habari hizo wanahaha kumzuia asiongee huku wakitaka kujua anataka kuongea nini na wanampango wa kuhakikisha aengei chochote na wameshambembeleza sana lakini amesimama kuwa kwenye msimamo wako kuwa ataongea kabla ya tarehe 24!

Zina fanyika kila juhudi za kunusuru tukio hilo kwani wanasema litasambaratisha umoja huo kabisa.

Lakini amesisitiza kuwa hayuko tayari kushiriki siasa za kinafiki kamwe...!

Je watafanikiwa kumzuia?
Ni nani huyo?
Ataendelea kukaa kimya?
Ni kwañini hawataki aongee?

Wana jamvi muda huongea tusubiri!

Karibuni wana jamvi!
Wewe kweli sio mke mwema. Yani unatoa sisi za mme wako hadharani. Jaribu kutunza siri za mmeo
 
ni furaha sana nyumbu mmoja akirudi kundini
 
Umesikia hao watu wanasema "Hapa kasi tu" Uelewe maana yake nini. Nani atakuwa na pesa mtaani?

Ha

Mkuu nakubaliana nawe. "Hapa kasi tu" inakamua maskini hadi shilingi ya mwisho. Mtaani hakuna pesa.

Mkuu wa nchi naye anajua hakuna pesa halafu anasema watu wafanye kazi, kazi zilizopo kwa sasa ni za u-DC,u-DAS,u-DED?

Lakini ili uzipate sifa yake lazima uwe kada wa CCM...
 
Mbowe: Kwenye mkutano wa 24 Julai tumepanga uongee, utapangiwa maneno ya kuongea
Mnyika: Nini? sitaki habari hizo

Salum Mwalimu: Si utaongea tu sheikh yaishe ...
Mnyika: Nimesema bradha siongei

Mdee: Mnyika usiongee kwa kulazimishwa kama zuzu
Mnyika: kimya

Mbowe: John unatikisa kiberiti?
Mnyika: kimya

Lowassa: Kama hatayaongea maneno niliyowaelekeza basi mimi nitaondoka.
Mnyika: huku akisonya anasema "Basi mimi nitaongea kabla ya 24 maneno yaliyo moyoni mwangu ili 24 na nyie muongee yenu"

Wote: Basi basi Mnyika usiongee
Mdee: Mnyika sawa ongea kabla
Mnyika: Nimeishaamua nitaongea siburuzwi
Wote: Usiongee usiongee

Hii ni muvi mpya Bavicha wanauzuia mkutano wa CCM na Mnyika analazimishwa kuongea na kutoongea.
 
Kwani wameondoka wangapi mbona nchi haikutikisika?kwani yeye Mungu? Siasa ni sehemu ya maisha yakikushinda unapisha wengine na maisha yanaendelea.
 
Picha lemeanza.Sterling hajajilikana bado watu wanagues.Ndindindindi yoli ndi.....[emoji123][emoji818]
 
JF ikiwekwa post hata kama ni porojo nimejifunza kutoidharau kwani Mwishoni mwa Mwezi July 2015 mpaka trh 6 September 2015 nilijifunza mengi, nilikuwa mbishi kuwa DR. hawezi kuondoka CDM sasa haya ya Mnyika.........
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom