saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
MBUNGE wa Jimbo la Mbogwe, Mhe. Nicodemus Maganga amesema watu wote waliohusika kwenye mkataba wa TANESCO na Symbion na kulisababisha Taifa hasara ya Bilioni 350 wakamatwe mara moja kwani watu wote waliohusika na kashfa hiyo wapo.
Maganga amesema hayo Novemba 4, 2022 bungeni Dodoma wakati akijadili Taarifa za Kamati za PAC, LAAC na PIC kuhusu Ripoti ya CAG ambapo amesema mkataba wa Tanesco na Kampuni ya Symbion ulioingiwa Septemba 2015 umeliingiza taifa kwenye hasara kubwa.
“Hawa watu wote wapo wakamatwe mara moja na hili zoezi ni dogo sana tukilikuza linakuwa kubwa lakini zoezi hili linaweza likamalizwa na mtu mmoja tena Waziri wa Mambo ya Ndani hili suala liko ndani ya uwezo wake mara moja tu akitangaza kesho waripoti Dodoma kwani shida iko wapi waripoti wenyewe kesho tuone trilioni zetu zote tukajenge barabara tufanye na mambo mengine maisha yaendelee” amesema Mhe. Maganga