PreGE2025 Mbunge Maganga: Bora niwe Chawa kwa Rais ili Wananchi wapone

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, Nicodemus Maganga, amesema yuko tayari kuwa "chawa kwa Rais" ili kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma muhimu za afya, elimu, maji na barabara.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Nanda kwenye mkutano wa hadhara, ambapo amekiri kuwa eneo hilo linakabiliwa na ukosefu wa kituo cha afya.

Maganga amesema kuwa kuna makosa mengi ambayo binadamu hufanya bila kujua, lakini kwa upande wake yuko tayari kufuata njia yoyote itakayosaidia kupata maendeleo kwa wananchi wake.

''Wakubwa wanataka heshima, ukienda umemdharau atakupa hela ya kituo cha Afya, atakupa hela ya barabara, ukiona namsifia Rais ujue mwishoni naelezea pia matatizo ya wananchi, uache kuwa chawa huna hela, niache kuwa chawa wa Rais niwe chawa wa nani? nimeacha wananchi laki nne kwenye Jimbo langu wengine wana nja, wengine hawana dawa kwanini nisiwe chawa ili wananchi wapate kupona"amesema Maganga akitumia lugha ya Kisukuma.

pesa za sa100 au ni kodi zetu?

#NoReformsNoElection
 
Back
Top Bottom