Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. MARTHA MARIKI ACHANGIA MILIONI 29 MAKUNDI YA AKINA MAMA MKOA WA KATAVI ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki ameendelea na ziara yake katika Kata mbalimbali za Mkoa wa Katavi huku akikabidhi Shilingi Milioni 29 za kuwawezesha wanawake kiuchumi kama mitaji ya kuendeleza shughuli zao.
Mhe. Martha Mariki Katika ziara aliyofanya ya kukagua Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Ilangu alitoa na kuchangia Shilingi Milioni Moja kama sehemu yake ya kuunga mkono jitihada za wananchi katika Ujenzi wa kituo cha Afya Ilangu
Katika ziara yake ya tarehe 10 Julai, 2023 Mbunge Martha alifanya Mkutano wa Hadhara katika Kata ya Ilangu na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 huku akiainisha miradi na mambo mazuri yaliyofanyika chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Serikali ya Awamu ya Sita
Aidha, Mhe. Martha Festo Mariki alifanya Mkutano wa ndani uliohusisha Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa ngazi ya Kata, Matawi, Mabalozi na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla na kuelezana mambo mbalimbali ya kiutendaji ya kuimarisha uongozi.
Vilevile, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki katika ziara hiyo alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Makazi Mishano
Mwisho, Wananchi na viongozi wampongeza Martha kwa kuwawakilisha na kuwasemea vizuri Bungeni huku wakimpa zawadi ya Kuku, Ndizi, Mahindi kama sehemu ya kutambua mchango wa Mbunge huyo kwa wananchi ambao wameonyeshwa kukubali utendaji wake na jinsi alivyojikita kuwainua kiuchumi wanawake.
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-07-12 at 06.53.51(1).jpeg133.8 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2023-07-12 at 06.53.49(1).jpeg113.1 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2023-07-12 at 06.53.50.jpeg113.1 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2023-07-12 at 06.53.50(1).jpeg158.5 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2023-07-12 at 06.53.48(1).jpeg148.7 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2023-07-12 at 06.53.50(2).jpeg178.8 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2023-07-12 at 06.53.54.jpeg112.7 KB · Views: 6