MBUNGE MARTHA MARIKI: AITAKA SERIKALI KUWEKA RUZUKU KWENYE MKAA MBADALA ILI WANANCHI WAUPATE KIRAHISI
"Nampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya nchini Tanzania. Nampongeza Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, Kamishna wa Madini na Watendaji wote wa Wizara ya Madini kwa kazi nzuri" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi
"Sekta ya Madini imeendelea kukua siku hata siku, leo hii Sekta hii imeweza kuchangia zaidi ya Asilimia 10.1 katika Pato la Taifa na hii ni kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kuweka jicho la kipekee kwenye sekta ya madini ambayo sasa imekuwa mkombozi kwa kuchangia ajira kwa akina mama pamoja na vijana"
"Uendelezaji Migodi kwa wachimbaji wadogo, Nampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa mitambo 15 kwaajili ya Uchorongaji, mitambo hii imeleta Mapinduzi katika sekta ya madini ambayo imegawanywa maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Naomba Wizara ya Madini, Wanawake watengewe baadhi ya mitambo na wakodishiwe kwa bei nafuu"
"Ufutaji wa Leseni, Nampongeza Waziri Mavunde; kulikuwa na Leseni zaidi ya 2648 zilizokuwa zimeshikiliwa na watu bila kuzifanyia kazi. Mpaka sasa kuna Leseni zaidi ya 58, nakuomba Waziri wa Madini watengee wanawake, nenda na akina mama katika uchimbaji wa madini"
"Utekelezaji wa ahadi za viongozi, kuna baadhi ya maeneo yapo kwenye hifadhi ikiwemo eneo la Kigosi yametolewa kwa wachimbaji wadogo wadogo. Changamoto ni Sheria ngumu kwenye haya maeneo ya hifadhi, naomba tuziangalie Sheria hizi, mfano kulipa fedha baada ya kukata mti"
"Mkaa Mbadala unakwenda kuleta Mapinduzi makubwa, niiombe sana Serikali kwa kushirikiana na STAMICO kuzidi kutoa elimu kwa akina mama kwani watu wanaoathirika sana kwa kutumia Nishati chafu ni akina Mama na tumesema ifikapo mwaka 2034 tunataka asilimia 80 ya Watanzania tuweze kutumia Nishati safi"
"Naipongeza Wizara ya Madini na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kazi nzuri tuliyofanya mpaka Wizara ya Madini imeweza kuongeza ukusanyaji wa Maduhuli ambapo Mwaka 2022/2023 tulikusanya Maduhuli zaidi ya Bilioni 678; Mwaka 2023/2024 tumekusanya Maduhuli bilioni 754 na Mwaka 2025 tunatarajia kukusanya Maduhuli zaidi ya Trilioni Moja na kufikia asilimia 66 ya lengo"