PreGE2025 Mbunge Martha Mariki akabidhi taarifa ya Utekelezaji Mkoa wa Katavi 2020 - 2025

PreGE2025 Mbunge Martha Mariki akabidhi taarifa ya Utekelezaji Mkoa wa Katavi 2020 - 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki tarehe 21 Mei, 2025 amekabidhi rasmi Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Mbunge kwa kipindi cha miaka mitano, 2020-2025 kwenye Baraza la UWT Mkoa wa Katavi.

Akizungumza wakati akiwasilisha Taarifa yake katika Baraza hilo, Martha Mariki amekabidhi pia Viti 600 vyenye thamani ya Shilingi Milioni Kumi na Mbili (12,000,000) kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Katavi kwaajili ya matumizi ya Ofisi na kama mradi wa kujiingizia mapato.

Aidha, Martha Festo Mariki akiwa katika Baraza la UWT Mkoa wa Katavi amekabidhi fedha shilingi milioni Nane (8,000,000) kwaajili ya Ujenzi wa Nyumba za watumishi (Makatibu) wa UWT Mkoa wa Katavi.

Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi amewasilisha Taarifa ya Utekelezaji mbele ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndugu Idd Kimanta; Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwamvua Mrindoko; na viongozi wengine Serikali na Chama (CCM, UWT, UVCCM na Wazazi) Mkoa wa Katavi pamoja na viongozi wa Wilaya za Mkoa wa Katavi.

Vilevile, Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa Baraza la UWT Mkoa wa Katavi, viongozi wa CCM na UWT wa Mkoa na Wilaya wamempongeza Martha Festo Mariki kwa kazi aliyofanya kwa kipindi cha miaka mitano ya uwakilishi wa Wanawake bungeni kwani wameona jinsi ambavyo amekuwa akiuliza maswali na kuchangia hoja kwa lengo la kuleta maendeleo Mkoani Katavi.

Mwisho, Martha Festo Mariki amewashukuru wana CCM na wana UWT Mkoa wa Katavi kwa kumpa ushirikiano mkubwa katika kipindi cha miaka mitano na amewaomba wamuunge mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa katika Uchaguzi Mkuu ifikapo Oktoba 2025.

WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.53 (1).jpeg
WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.55.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.53 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.53 (2).jpeg
    671.9 KB · Views: 33
  • WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.54.jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.54.jpeg
    786.4 KB · Views: 35
  • WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.53.jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.53.jpeg
    745.8 KB · Views: 35
  • WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.54 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.54 (1).jpeg
    98.8 KB · Views: 33
  • WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.55 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-22 at 10.46.55 (1).jpeg
    538.6 KB · Views: 45
Back
Top Bottom