Nimefuatilia kwa makini thread ya mbunge wa viti maalum, Martha Mlata.
Mimi binafsi nimekutana na huyu mama, ni mwenyeji wa Singida.
Hakufanikiwa kupata elimu ya juu (A-level+university).
Akabahatika kuolewa na Dr. wa hapo UDSM. Kwa kumwangalia mama ni mzuri kwa kweli tusifu uumbaji. Vigogo hawawezi kuvumilia pindi akiwapitia karibu.
Maisha ya honeymoon yalikuwa mazuri tu, ila baada ya kupata mtoto wa pili, maisha yalianza badirika, ukichanganya Dr. kujenga nyumba ya ghorofa, ikawa shida moja kwa moja.
Ndoa iliingiliwa na ndugu, huyo "Dr. ni NSHOMILE" mnawajua hawa ndugu zetu. Hata kwenye sherehe wewe kama huna jina la kihaya utaambulia kunywa maji ya chupa, wakikuheshu sana.
Dr. akaambiwa aowe mhaya, martha siyo mke. sijui Dr. naye karogwa!! akaanza kumfanyia vituko, kumpiga hata kutaka kummuua huyu mama.
Hii ndiyo iliyomtoa Martha ktk ndoa yake. Dr. akachukua vitoto kuvipeleka boarding school, na kumwekea mama wanted kuona watoto.
Martha asili yake ni mwimbaji kwaya kanisani, ndiko alikotokea kabla ya kuolewa, hata baada ya ndoa yake Martha aliendelea kumwimbia Mungu. Huenda huko ndiko Mungu alikomtoa na kumweka hapo alipo.
Binadamu tuna mapungufu mengi tu, lakini tukipatiwa nafasi nadhani kila mmoja wetu anaweza akafanya vizuri.
Binafsi naona hatua aliyochukua huyu mama ya kwenda masomoni inaonyesha kweli she need a change. Huenda kutokuwa na elimu pia kulipelekea ndoa yake kwenda mlama. ingawa hata wasomi ndoa zao zinamatatizo.
Wabunge VIHIYO ni wengi sana bungeni, issue je wanatumiaje nafasi hii kujinasua ktk hali ya uvihiyo? Je ipi inapendeza, kwa Martha kwenda shule au kwa John Komba nawengine kununua degrees?
Hadija Kopa ni mjumbe wa NEC Je ana elimu na uwezo gani wa kutuchagulia Rais?? na wengine wengi tu.
Uliyekerwa na Martha kwamba hahudhurii shida na sherehe za watu, ni vyema ukamwambia, kuliko kumzungumzia ubaya. Kila mtu ana uhuru wa maisha yake.
Wa-Tanzania, mara zote mke anaposhindwa kuvumilia yanayomsibu ndani ya nyumba, aondokapo basi lawama anarushiwa yeye, kwamba amekimbia ndoa na kwenda kufanya umalaya. Akina mama wengine wamefikia hata kuuawa na waume zao, kwa kungángánia kulinda heshima ya ndoa.
Ni wamama wengi wanapitia maisha ya kunyanyaswa ktk ndoa zao, wengi wanakata tamaa, wanaoinuka na kuendelea na maisha ni jambo la kuwapongeza.
Jamani tubadirike na tujifunze kuheshimu maamuzi ya wenzetu, bado tuna nafasi ya kuwashauri wale wanaohitaji mawazo. Tuwape nafasi wale walioathirika na mfumo dume wa maisha, ndiyo maana hii JF inatufunza mengi. Na kupitia hii JF tunaupiga vita ufisadi, tunajifunza jinsi ya kuwapenda na kuwasaidia wenzetu, wasio na ajira wanapatiwa links za ajira n.k.
Asante.