Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
Bungeni Dodoma 📍
May 2, 2025.
Katika kuchangia bajeti ya wizara ya madini Mbunge wa lupa Mh Masache Kasaka ameomba serikali kupitia wizara hiyo kuweka utaratibu mzuri wa wataalam wa kigeni kutokuingilia shughuli za wazawa katika maeneo ya uchimbaji na badala yake kufanya yale yaliyowaleta.
Sambamba na hilo Mh Masache Kasaka ameomba serikali kutimiza ahadi iliyotolewa mwaka jana 2024 ya kununua ndege itakayo wezesha utafiti iweze kununuliwa kupitia bajeti ya 2025/2026 ili kupunguza hasara kwa wachimbaji wadogo katika maeneo wanayofanya shughuli za uchimbaji.
katika hoja nyingine Mh Masache Kasaka ameishauri serikali kuweka chombo kimoja cha ukusanyaji tozo badala yake kufanya ya kila sekta kukusanya tozo kwa wachimbaji wadogo ambayo ineleta hasara kwa wachimbaji hawa.
KAZI NA UTU
CHUNYA TUNASONGA MBELE