PreGE2025 Mbunge Mashimba Ndaki akabidhi Magari ya wagonjwa Malampaka na Mwabayanda jimboni mwake

PreGE2025 Mbunge Mashimba Ndaki akabidhi Magari ya wagonjwa Malampaka na Mwabayanda jimboni mwake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Makabidhiano ya magari hayo yamefanyika kwa nyakati tofauti tofauti katika vituo hivyo yamefanywa na Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,mbunge Ndaki amewataka wananchi na waganga wafawidhi wa vituo hivyo kuyatunza magari hayo na kuyawekea utaratibu mzuri wa matumizi.

Amesema kuwa ni vizuri magari hayo yakaegeshwa katika maeneo ya vituo hivyo na siyo katika hospitali ya wilaya ya Maswa.

"Siku ya leo tunayofuraha kubwa ya kupata gari la wagonjwa katika kituo chetu cha Malampaka na Mwabayanda sina budi kuishukuru serikali kwa kutupatia magari hayo mapya kutokana na umuhimu wa vituo vyetu hivyo ambavyo vinahudumia maeneo mapana ya wilaya ya Maswa na nje ya mkoa wetu wa Simiyu,”amesema.

Magari hayo yamenunuliwa na serikali kwa gharama ya Sh Milioni 200 kila moja ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma za afya hapa nchini.
IMG_1368.JPG
IMG_1520.JPG
 
kiinua mgongo milioni mia tano unatoa hapo vimilioni 50 unachukua chuma used unaenda kutoa msaada mbwembwe kibaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaao , kwakweli watanzania tumerogwa, na ikumbukwe kuwa qualification za mbunge ni kusoma na kuandika tu over, Haya tusubirie maendeleo kwa majirani zetu.
 
Hizo si gari za serikali imekuaje mbuge kazitumia kisiasa kuwa yeye ndo katoa msaada?
 
Back
Top Bottom