Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MAVUNDE AAHIDI UJENZI WA KIVUKO KINACHOUNGANISHA KATA YA MSALATO NA MIYUJI
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akiongozana na Diwani ya Kata ya Msalato Mh. Nsubi Bukuku kukagua eneo la kivuko kinachotakiwa kujengwa katika Mtaa wa Senje kuunganisha kata ya Msalato na Miyuji.
Wakizungumza na Mbunge Mavunde ,wananchi hao walimshukuru Mbunge Mavunde kwa kusaidia ukarabati wa barabara katika mtaa wa Senje na kumuomba kuwasilisha changamoto hiyo TARURA kwa lengo la kupata ufumbuzi wa tatizo la kujaa maji katika eneo hilo ambao kipindi cha masika halipitiki kirahisi na hivyo kupeleka adha kwa wanafunzi wengi waliopo katika eneo hilo.
Akijibu hoja za wananchi Mbunge Mavunde ameahidi kukaa na TARURA kutafuta ufumbuzi wa muda kutatua adha hiyo kabla ya kuja na ufumbuzi wa kudumu wa kuondoa changamoto hiyo.
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-07-22 at 08.41.33.jpeg92.4 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-07-22 at 08.41.34.jpeg133.6 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-07-22 at 08.41.35.jpeg111.9 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-07-22 at 08.41.35(1).jpeg123.5 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2024-07-22 at 08.41.36.jpeg212 KB · Views: 8 -
WhatsApp Image 2024-07-22 at 08.41.36(1).jpeg177.8 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2024-07-22 at 08.41.37.jpeg121.4 KB · Views: 8