Mbunge Mligo: Tanzania Moja, Serikali Moja, Lakini tuna Mifumo Miwili ya Elimu ambayo inayoumiza Vijana

Mbunge Mligo: Tanzania Moja, Serikali Moja, Lakini tuna Mifumo Miwili ya Elimu ambayo inayoumiza Vijana

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kwa sababu bila kuumiza kichwa zaidi naanza mfano kwenye issue ya elimu ni Tanzania moja ni serikali moja tuna mifumo ya elimu ya aina mbili mtoto wa waziri wa mbunge amesoma English medium mfumo wa kiingereza mtoto wa mama anasoma kwenye shule ya msingi ambao mfumo ni wa kiswahili tunatarajia wakimaliza wakashindane kwenye soko kwenye interview moja mlango mmoja kwenye interview moja mlango mmoja vitu kama hivi muhimu hatuzungumzi hapa huyo huyo mwananchi wa kawaida leo hii mmesema wana mikopo ya 10% ndio mmesema kuna bilioni 18"

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Njombe kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Sigrada Mligo amezungumza hayo wakati akitoa hoja Bungeni, wakati wa uwasilishwaji wa bajeti ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, leo Juni 1, 2026.

 
SAFI SANA ANGALAU AMEONGEA POINT KULIKO HAWA KUMSIFIA MAMA
 
Mfumo wa elimu nchini umeparanganyika, kila mwananchi atasomesha mtoto wake kutokana na hali yake ya kiuchumi. Diwani tu wa kata mtoto wake hasomi shule ya kata othewise huyo diwani uchumi wake ni mdogo. Miaka ya nyuma enzi za mwinyi, mkapa watoto wa vigogo wote wakubwa walisoma pamoja na watoto wa wananchi wa kawaida. Leo kuna shule za walalahoi na shule za wenye nacho, mifumo miwili ya shule
 
Back
Top Bottom