Mbunge Morogoro Achangia Milioni Tatu Wakulima wa Mpunga Kilombero

Mbunge Morogoro Achangia Milioni Tatu Wakulima wa Mpunga Kilombero

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE MHE. NORAH MZERU ACHANGIA MILIONI 3 VIKUNDI VYA WAKULIMA WA MPUNGA KILOMBERO

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mhe. Norah Waziri Mzeru amechangia Miradi ya Kimaendeleo ya wanawake wa Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilombero Kata za Mang'ula A; Mang'ula B na Kata ya Kibelege Shilingi Milion tatu (Tsh 3,000,000/)

Mhe. Norah amechangia ikiwa ni Miradi ya Ulimaji wa Mpunga ambayo Vikundi vitatu vya Wanawake Wilayani Kilombero Wameanzisha miradi Mikubwa ya Kilimo cha Mpunga huku akifurahishwa sana na Uchapakazi wa Wanawake wa Kilombero katika Mradi wao wa Mpunga ambao Umeshamiri.

Sambamba na hilo Mhe. Norah Waziri Mzeru Amesema "Wanawake tunakila sababu ya kusimama vifua mbele katika maswala ya maendeleo, tuendelee kuongeza Ubunifu katika Miradi bila kuogopa kwani Rais wa JMT Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza kila Siku juu ya Wanawake Kukua Kiuchumi na Uchumi wetu Utakua kwa Kuwa na Miradi Mbalimbali Kama hii ya Kilimo"

"Dhamira kubwa ya kimaendeleo ambayo Rais wa JMT Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayoionesha katika Taifa letu kwa Kuleta Mvua nyingi za Maendeleo Kwenye Kila Sekta mfano, Kulipa Malimbikizo na Madai kwa Walimu, Utalii Umeongezeka, Nchi yetu Imefunguka, Demokrasia imekua, Kuondolewa kwa tozo ya VRF, Shule Mpya 266, Madarasa Mapya zaidi ya 23,000, Mabweni Mapya 170 , Vyoo Vipya 568, Ajira zaidi ya 38,700 na mambo mengine mengi"

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kujipambanua vyema katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Kasi kubwa sana, hivyo kama wanawake na Watanzania kwa Ujumla tuendelee Kumuunga Mkono kwa Kushiriki Shughuli Mbalimbali za Kiuchumi kama wanawake wa Kilombero Mnavyo Shiriki Kupitia Miradi yenu mikubwa ya Mpunga.

Mwisho, Mhe. Norah Waziri Mzeru (Mbunge) Aliwasihi Wanawake Kuwa Macho na Kuwalinda watoto wao wa Kiume na Wakike ili Kupunguza Ukatili wa kijinsia kwa Watoto.

Ofisi ya Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro
Mhe. Norah Waziri Mzeru


WhatsApp Image 2023-04-26 at 19.38.57.jpeg
WhatsApp Image 2023-04-26 at 19.38.54(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-26 at 19.38.53(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-26 at 19.38.53.jpeg

WhatsApp Image 2023-04-26 at 19.38.56(1).jpeg
 
Back
Top Bottom