Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mbunge wa Iringa Mjini Jesca Msambatavangu ameiuliza Serikali kuwa imejipanga vipi kudhibiti kile alichokiita kuwa wizi wa binadamu (utekaji) nchini Tanzania. Swali hilo lilielekezwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi na lilitakiwa kujibiwa na Naibu Waziri Daniel Sillo. Lakini Spika wa Bunge Dkt. Tulia akatoa maelekezo kuwa swali hilo inatatuliwa liwasilishwe kama swali la msingi ili serikali iweze kulitolea majibu.