Elections 2010 Mbunge mteule wa Karagwe anajuta

Wakubwa mimi niko against wizi wa kura, na imeniuma sana ukizingatia jimbo nililopiga kura na mbunge niliyempigia walimchakachulia matokea yake, lakini hii ishu ya watu kuwawinda watu na kuwakimbiza maeneo yao ya kuishi si sawa kabisa na wala hatutakiwi kuishabikia kwa namna yoyote ile. NIna sababu zifuatazo:
1. Sio kila anayeshinda uchaguzi anapendwa na watu wote. This means hata pale unapopata zaidi ya 60% kuna 40% watakaoukuwa wameumia kwa njia moja au nyingine, hivyo wakiamua kuonyesha hasira zao kwa madai waliibiwa hata kama sio kweli hii nchi haitakalika
2. Hao watu wanaowinda hao walioshinda, dont tell me ni Karagwe nzima au Shinyanga mjini nzima, ni kikundi tu cha watu wachache naweza kuwaita BANDITS ndo wanafanya hayo, idadi inaweza kuwa 20 au 100, lakini tusipoangalia tunaambiwa ni wananchi wa jimbo husika kama vile ni wote.
3. Hii pia inaenda kwenye majimbo mengine ambayo huwa tunayasifia, kwamba wananchi wanawapenda viongozi wao. Mifano nimesikia kwa Mwakyembe Kyela na hata kwa Mwandosya Rungwe sijui magharibi, "wananchi" huwaita wale wanaotaka kuwapinga hawa mabwana either ndani ya chama au kwenye jimbo (kupitia upinzani) na kuwakaripia waache nia hiyo. Hawa tunaowaita wananchi ni kina nani??? Kama ni wananchi wote kwanini wana ogopa huyu mtu kugombea? si wangeacha then wamthibitishie kwamba huyu ndio chaguo lao kwenye sanduku la kura????? NI rahisi sana kwa mgombea kukodi hao ninaowaita BANDITS kuwadhalilisha na kuwatisha wapinzani wake ili tu apite bila kupingwa ambayo ni mbaya tu kama kuchakachua.

Nikishasema hayo, narudia kusema pamoja na kwamba siafiki matumizi ya wizi wa kura etc, lakini pia sintaafiki matumizi ya nguvu eti ya "wananchi" kuwatishia hao wanaosemekana walishinda kwa kuiba kura au kuwashindisha watu kwa kuwaibia kura. Tuangalie jinsi ya kurekebisha matatizo yetu kwa kutumia njia sahihi...
 

Mbona Moshi vijijini au majimbo ya same na mwanga hakuna malalamiko? Wananchi wana majibu ya kura za kwenye vituo, wanajua kuandika na kuhesabu, kwa elimu yao duni ya darasa la saba majibu ya matokeo ya kwenye vitu yanaonyesha kashinda mgombea "A" lakini tume inamtangaza mgombea "B"; wakae kimya bila kuonyesha hisia zao?
 
a.k.a MiMi😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:😛eace:
 
mi nafikiri tanzania kuna wabunge wa aina tatu MMBUNGE WAKUCHAGULIWA NA WANACHI,MBUNGE WAKUTEULIWA,NA MBUNGE WAKUCHAKACHULIWA walioiba kura kupitia nec mbaya zaidi raisi pia WA KUCHAGULIWA NA KUCHAKACHULIWA
 

Asiwe na shaka akumbuke maneni ya busara ya Katibu Mkuu wa CCM (Mr. Makamba) kuwa "wananchi watasahau" na watamkubali baada ya muda mfupi ujao.
 

You have a point.

Muasisi wa uchakachuaji Tanzania ni marehemu baba wa taifa Mwl. Nyerere. Nakumbuka katika hotuba zake aliifananisha CCM na kokoro linalovua samaki na uchafu wote wa ziwani na pia alisema kuwa inanuka kwa rushwa. Lakini akamalizia kuwa lazima kiongozi bora atoke CCM. Mimi bado ninajaribu kutafakari alikuwa na maana gani kwani nikiangalia CCM na mfumo wake wa sasa wa kifidadi wa kuteuwa wagombea wake sioni uwezekano wa kiongozi bora kutokea kwenye hicho chama kwa siku za hivi karibuni.
 

i like that (red font)
 
Well said!
 
DC, RC, RPC, OCD, hawa kwa kuwa tunakaa nao pale Kayanga na Bukoba mjini, tutawashughulikia mmoja baada ya mwingine! Tuna ziwa Victoria na Mto Kagera, aliyeshuhudia wanyamulenge kwenye miaka ya 1994 awasimulie hawa jamaa, kwetu kuona mishikaki inaelea majini ni jambo la kawaida! We are feed up men! We are ready to be called tutus/hutu/nyakore than being called Tanzanian under the rule of JK charlatan!
 
Yule mzee alikuwa jasusi,kabebeshwa sifa asizostahili kuwa nazo,Mandela, Arafat wana Nobel Prize how about him? ni kwa sababu ya tabia za kijasusi alizokuwa nazo!
 
Kama mtu hakuwepo Tanzania tokea 30/10/2010 na kwamba alienda sehemu ambayo hakuna mawasiliano na sasa amerudi. Bila shaka atajiuliza; je, ni ndoto au ni kweli kwa Tanzania?

My God! Kama ni mimi ndo huyo mbunge, naurudisha ubunge MARAMOJA, nakujiunga na wananchi kutafuta mbunge mwingine huku nikiwaomba msamaha kwa usumbufu wowote.
 
Hawezi kuwa yupo jimboni kwa vyovyote atakuwa Dodoma Kuwahi sehemu ya kuishi. ila kama ni kweli hao watu wamefanya siasa hizo basi siungwana na lazima wasakwe wote na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kama wanafikiri kuna ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi zilizompendelea huyo mbunge mteule ni vizuri wakawahi mapema mahakamani kudai haki yao. Utaratibu wanaoufanya haukubaliki
 

Nimetoka tarime leo,hali inaweza isiwe sawa na huyo jamaa ila mbunge mteule wa kule hawezi tembea hivi hivi kama wenzake walivo zoeleka kujichanganya na watu!
Na hajakaa sana tarime toka achaguliwe nadhani atarudi 2014 kujiandaa na kampeni 2015
 
Big up wananchi wa karagwe. Hili ni fundishokwa wezi wote wa kura.
 

Naunga mkono moja kwa moja maoni yako. Kumbuka ni Nyerere huyohuyo aliyesababisha vita na Uganda baada ya kuwahifadhi wapinzani wa Amini na kuwapa fursa kumpinga wakitokea Tz, ndo amini akaona heri aivamie na Tz kumuadabisha Nyerere, bahati mbaya mamia ya ndugu zetu walikufa. Pia 2015 mamia ya waTz watauliwa na police watakapoamua kufa kwa ajili ya nchi yao baada ya mtindo aliouanzisha Nyerere kuendelea kwa waTZ kuendelea kuibiwa kura zao na kuchaguliwa mafisadi kuendelea kuwaongoza
 
mchakachuaji1, ni vibaya sana kumsema vibaya mtu ambaye hawezi kujitetea! Wach roho ya JK wa kweli ilale mahali pema ilipo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…