Mbunge Mulamula afurahia kupanda Coaster

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Dodoma. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Liberata Mulamula ametaja kilichomfurahisha kwenye ziara za kamati kuwa ni basi aina ya Toyota Coaster.

Mulamula ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Februari 1, 2023 wakati akichangia taarifa za kamati, ambapo amesema hakuwa amepanda usafiri huo.

Mbunge huyo amesema kwake kupanda usafiri huo akiwa na wanakamati wenzake ilikuwa ni kitu kipya ingawa alifurahia usafiri wa namna hiyo.

Kingine ameliambia Bunge kuwa leo ni mara yake ya kwanza kusimama akiwa 'back bencha' (mbunge wa kawaida) ambapo pia ameeleza furaha yake kuwa amepokewa vema.

"Kila wakati ni kushukuru na kila jambo ni kushukuru, naomba nishuruku namna Spika alivyonipokea na kunipangia kamati ya Viwanda na Biashara, namshukuru sana pamoja na viongozi wa kamati yetu," amesema Mulamula.

Katika mchango wake mbunge huyo ametaja wananchi kutambua hakuna kitu kikubwa kilichoanza kwa ukubwa bali kila kitu kilianza kwa udogo wake.

mula_mula_balozi_bungeni_700_466shar-50brig-20.jpg

Source: Mwananchi online
 
Huyo labda kama anamzungumzia mtu ambae ni mpenzi wake wa jinsia yake otherwise hana ujumbe wowote zaidi ya kujiona bwege hajiamini
 
Dodoma. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Liberata Mulamula ametaja kilichomfurahisha kwenye ziara za kamati kuwa ni basi aina ya Toyota Coaster.
Mulamula ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Februari 1, 2023 wakati akichangia taarifa za kamati, ambapo amesema hakuwa amepanda usafiri huo.

Mbunge huyo amesema kwake kupanda usafiri huo akiwa na wanakamati wenzake ilikuwa ni kitu kipya ingawa alifurahia usafiri wa namna hiyo.
Kingine ameliambia Bunge kuwa leo ni mara yake ya kwanza kusimama akiwa 'back bencha' (mbunge wa kawaida) ambapo pia ameeleza furaha yake kuwa amepokewa vema.

"Kila wakati ni kushukuru na kila jambo ni kushukuru, naomba nishuruku namna Spika alivyonipokea na kunipangia kamati ya Viwanda na Biashara, namshukuru sana pamoja na viongozi wa kamati yetu," amesema Mulamula.

Katika mchango wake mbunge huyo ametaja wananchi kutambua hakuna kitu kikubwa kilichoanza kwa ukubwa bali kila kitu kilianza kwa udogo wake.
Source:mwananchi online
"Mbunge huyo amesema kwake kupanda usafiri huo (wa basi) akiwa na wanakamati wenzake ilikuwa ni kitu kipya ingawa alifurahia usafiri wa namna hiyo"

Mhh! Kijembe hiki kwa mwezake kutokana na bifu la kina mama.
 
Dodoma. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Liberata Mulamula ametaja kilichomfurahisha kwenye ziara za kamati kuwa ni basi aina ya Toyota Coaster...
Eeeh kumbe huyu mweupe hivi kichwani, Mh. Rais alifanya vema sana kumtoa, hamna kitu kabisa huyu, hivi hawa watu ni akili zinapungua au?
 
Back
Top Bottom