Mbunge Mulamula afurahia kupanda Coaster

Mbunge Mulamula afurahia kupanda Coaster

Dodoma. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Liberata Mulamula ametaja kilichomfurahisha kwenye ziara za kamati kuwa ni basi aina ya Toyota Coaster.

Mulamula ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Februari 1, 2023 wakati akichangia taarifa za kamati, ambapo amesema hakuwa amepanda usafiri huo.

Mbunge huyo amesema kwake kupanda usafiri huo akiwa na wanakamati wenzake ilikuwa ni kitu kipya ingawa alifurahia usafiri wa namna hiyo.

Kingine ameliambia Bunge kuwa leo ni mara yake ya kwanza kusimama akiwa 'back bencha' (mbunge wa kawaida) ambapo pia ameeleza furaha yake kuwa amepokewa vema.

"Kila wakati ni kushukuru na kila jambo ni kushukuru, naomba nishuruku namna Spika alivyonipokea na kunipangia kamati ya Viwanda na Biashara, namshukuru sana pamoja na viongozi wa kamati yetu," amesema Mulamula.

Katika mchango wake mbunge huyo ametaja wananchi kutambua hakuna kitu kikubwa kilichoanza kwa ukubwa bali kila kitu kilianza kwa udogo wake.

mula_mula_balozi_bungeni_700_466shar-50brig-20.jpg

Source: Mwananchi online
Nimefurahi kula mhogo leo, kumbe mtamu.
Nilikuwa nakula keki kila siku.
 
..Ni mama ana mume na watoto.

..ziko mpaka video clips akimtambulisha mume wake.

..kuna wachangiaji wanatumia vibaya mitandao kuchafua wengine.
Kwani wa Mama ambao wana watoto na mume hawana wapenzi wa jinsia yao?
 
Dodoma. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Liberata Mulamula ametaja kilichomfurahisha kwenye ziara za kamati kuwa ni basi aina ya Toyota Coaster.

Mulamula ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Februari 1, 2023 wakati akichangia taarifa za kamati, ambapo amesema hakuwa amepanda usafiri huo.

Mbunge huyo amesema kwake kupanda usafiri huo akiwa na wanakamati wenzake ilikuwa ni kitu kipya ingawa alifurahia usafiri wa namna hiyo.

Kingine ameliambia Bunge kuwa leo ni mara yake ya kwanza kusimama akiwa 'back bencha' (mbunge wa kawaida) ambapo pia ameeleza furaha yake kuwa amepokewa vema.

"Kila wakati ni kushukuru na kila jambo ni kushukuru, naomba nishuruku namna Spika alivyonipokea na kunipangia kamati ya Viwanda na Biashara, namshukuru sana pamoja na viongozi wa kamati yetu," amesema Mulamula.

Katika mchango wake mbunge huyo ametaja wananchi kutambua hakuna kitu kikubwa kilichoanza kwa ukubwa bali kila kitu kilianza kwa udogo wake.

mula_mula_balozi_bungeni_700_466shar-50brig-20.jpg

Source: Mwananchi online
Komwe lile!!!!
 
Kamjibu Mtu hapo kuwa hata Yeye alivyopanda Basi Mazishini nchini Uingereza hakupaswa Kukasirika na kuishia Kumtumbua.
Tena ameenda mbali zaidi kwa kusema hakuwahi kupanda usafiri huo ila ameufurahia mno.

Hebu tujiulize;
1. Je ni kweli Liberata hajawahi kupanda basi katika ukuaji wake? Maana hawa wasomi wa zamani wamesafiri sana kwa mabasi ya railway.
2. Je coaster ina tofauti sana na aina nyingine ya usafiri?
3. Kwamba katika yote yeye kilichomfurahisha ni kupanda coaster tu.

Ujumbe hapa ni kuwa;
1. Hili ni dongo kwa mtu fulani, pengine walianza kutofautiana pale mama alipopandishwa basi na kisha picha kuenea akiwa ndani ya basi hilo.
2. Kwamba kitendo kile kwa libarata kilikuwa cha kawaida sababu marais wengine nao walipanda mule. Lakini kumbe mama alitaka kuwa treated very special. Maana hata waziri mkuu wa Ethiopia alitumia magari ya ubalozi.
3. Liberata alifanya kazi na mtu asiyemjua tena mswahili haswa. Cha muhimu atulie tu kwa sasa maana jumbe kama hizo zikiwafikia chawa itakuwa shida. Japo ujumbe umetolewa kisomi.
 
. Liberata alifanya kazi na mtu asiyemjua tena mswahili haswa. Cha muhimu atulie tu kwa sasa maana jumbe kama hizo zikiwafikia chawa itakuwa shida. Japo ujumbe umetolewa kisomi.
Hebu tueleweshe ni usomi gani uliotumika hapo?
 
Mtu mwenye uraia wa Mareeeekan aliwezaje kuwa waziri wetu kinyume na Katiba?

Tuandike tu Katiba mpya na tuweke mifumo thabiti kuisimamia.

Aamen
 
Back
Top Bottom