Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe, ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita kwa kusikiliza na kutekeleza maoni ya wananchi kuhusu reforms za uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza bungeni leo, Aprili 11, Munde amesema: "Naipongeza Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Serikali sikivu chini ya Rais Samia. Watu waliongea mengi kuhusu uchaguzi na mpaka leo wanaendelea kuzungumzia reforms. Reforms zipo na zinaendelea kufanyika."
Ameeleza kuwa moja ya hatua kubwa zilizochukuliwa ni kubadilisha mfumo wa usimamizi wa uchaguzi. "Hapo awali wasimamizi wa uchaguzi walikuwa Wakurugenzi wa Halmashauri, lakini sasa Serikali imetangaza nafasi za kazi kwa wasimamizi wa uchaguzi kote nchini. Watafanyiwa usaili na kuchujwa, na wale watakaothibitika kufaa ndio watakaosimamia uchaguzi."