Mbunge Musukuma ashauri V8 za Mawaziri zifungwe mitungi ya gesi ili kubana matumizi

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Mbunge wa Geita Msukuma ameishauri serikali Kufunga mitungi ya gesi kwenye magari yote ya mawaziri ili kubana matumzi.

Ameyasema hayo leo hii 25/04 Bungeni wakati akichangia Bajeti ya wizara ya nishati.

Kwa sasa magari ya mawaziri, gari moja yaani V8 ikitoka Dar kwenda Dom inatumia laki 5 gharama ya mafuta tu.. endapo watafunga mitungi ya gesi tripu moja watatumia Sh. elfu 90.

Kama ni kweli basi naunga mkono hoja, na tunaiomba serikali Ibane matumizi kwa kufunga mitungi ya gesi magari yote ya serikali.

Nchi yetu/ watu wake bado ni masikini, hivyo suala la kubana matumizi Serikalini ni jambo muhimu sana.

Ila kuna baadhi ya watendaji hawana uchungu wala huruma, hawajali kama nchi hii bado ni masikini.....wabinafsi.

Pia soma
- Naibu Waziri Mkuu: Magari ya Serikali yafungwe mfumo wa gesi asilia
 
Watu tunapiga kelele magari ya serikali mwisho cc1990 msukuma analeta hoja zisizo na tija!
Kwani gesi inawekwa ile ya kupupu!
Tanzania inahitaji kuboresha mtandao wa bullet trains magari yabaki kwa short safaris. mf kiongozi atumie gari la serikali (dogo) lililopo kule anapofikia!
Hivi Tanzania tuna tatizo gani na sifa za migari ya SUV?
Utadhan Toyota wana kipengere maalum wakati tunapewa uhuru!
 
Mbunge wa Geita Msukuma ameishauri serikali Kufunga mitungi ya gesi kwenye magari yote ya mawaziri ili kubana matumzi.

Ameyasema hayo leo hii 26/04 Bungeni wakati akichangia Bajeti ya wizara ya nishati.

Kwa sasa magari ya mawaziri, gari moja yaani V8 ikitoka Dar kwenda Dom inatumia laki 5 gharama ya mafuta tu.. endapo watafunga mitungi ya gesi tripu moja watatumia Sh. elfu 90.

Kama ni kweli basi naunga mkono hoja, na tunaiomba serikali Ibane matumizi kwa kufunga mitungi ya gesi magari yote ya serikali.

Nchi yetu/ watu wake bado ni masikini, hivyo suala la kubana matumizi Serikalini ni jambo muhimu sana.

Ila kuna baadhi ya watendaji hawana uchungu wala huruma, hawajali kama nchi hii bado ni masikini.....wabinafsi.

Pia soma
- Naibu Waziri Mkuu: Magari ya Serikali yafungwe mfumo wa gesi asilia
NILIDHANI anashauri SERIKALI inunue magari yenye gharama nafuu za kuyaendesha kuliko hayo Ma V8
 
Ni bora wayauze ma vi8 yote wanunue IST zilizofungwa mitungi ya gesi.
 
Hakuna mwenye huruma kika anaye teuliwa anawaza kutumia V8, hawajali kama kuna wananchi masikini wanao hitaji huduma ya maji safi na madawa hospitalini
 
BUNGENI: Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amesema ili kuhakikisha Serikali inabana matumizi, ianze kuweka Mifumo ya Gesi katika Magari ya Viongozi wakiwemo Mawaziri, hali itakayosaidia kuokoa Fedha za Walipa Kodi.

Akichangangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati, Musukuma amesema "Gari kama V8 kutoka Dodoma hadi Dar utatumia kama 500,000, lakini ukitumia Gesi utatumia Tsh. 94,000 kwenda na Kurudi. Sasa kwasababu tunangaika na Matumizi makubwa ya Serikali, V8 zote zifungwe Mfumo wa Gesi".

Aidha, Mbunge huyo amehoji sababu za kusuasua kwa uwekezaji kwenye Vituo vya Kujaza Gesi ambapo amesema Wenye Magari wanatumia takriban Saa 9 kukaa kwenye Vituo wakisubiri huduma kutokana na uchache wa Vituo.
 
Kwa mbaali inaweza kuwa kama kukutana na mtu aliyetoka kununua Ferrari SF90 na kumpa “ushauri wa bure” afunge mtungi wa gesi kuokoa gharama kubwa ya petroli 🤔
 
Unafunga gesi kuokoa 406,000 afu mtu huyo huyo uliemfungia gesi anaiba 10,000,000,000 na hamna cha kumfanya si bora muache na gari lifaidi mafuta litakula wapi sasa limeumbiwa kunywa kiwese.
 
BUNGENI: Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amesema ili kuhakikisha Serikali inabana matumizi, ianze kuweka Mifumo ya Gesi katika Magari ya Viongozi wakiwemo Mawaziri, hali itakayosaidia kuokoa Fedha za Walipa Kodi.

Akichangangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati, Musukuma amesema "Gari kama V8 kutoka Dodoma hadi Dar utatumia kama 500,000, lakini ukitumia Gesi utatumia Tsh. 94,000 kwenda na Kurudi. Sasa kwasababu tunangaika na Matumizi makubwa ya Serikali, V8 zote zifungwe Mfumo wa Gesi".

Aidha, Mbunge huyo amehoji sababu za kusuasua kwa uwekezaji kwenye Vituo vya Kujaza Gesi ambapo amesema Wenye Magari wanatumia takriban Saa 9 kukaa kwenye Vituo wakisubiri huduma kutokana na uchache wa Vituo.
View attachment 2973510
Ameshafikiwa, amewezeshwa, maana speech yake ya mwisho kuhusiana na hili la magari kufungwa mifumo ya gas aliliponda vibaya sana sasa amegeuka ?
 
Sasa katk chagizo hilo lipaswa kupitshwa wawek station gesi kila mkoa /wilaya na bungen kwao maisha yaendeleee
from 500,0000/- to 94000/-

🔥
 
Back
Top Bottom