Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Musukuma, leo Machi 6, 2025, ameonesha magari 10 ya kubebea wagonjwa pamoja na moja kwa ajili ya Jeshi la Polisi, ambayo atawakabidhi wananchi wa jimbo lake ili kuboresha huduma za afya na usalama wa jamii.
Musukuma amesema magari hayo yatanufaisha wananchi wa Geita Vijijini, ambayo ina jumla ya kata 15, ambapo kila kata itanufaika na gari moja la kubebea wagonjwa. Aidha, ameeleza kuwa atagharamia mishahara ya madereva pamoja na matengenezo yote ya magari hayo. Wananchi watakaohitaji huduma watapaswa kuwasiliana na Katibu wa Chama kwa ajili ya uratibu wa usafiri.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Soma Pia: Kuelekea 2025 - Orodha ya CV za Wabunge kwa mwaka 2020 - 2025 kutoka kila mkoa Tanzania
Mbunge huyo pia amefichua kuwa gharama za mradi huo, ikiwemo ujenzi wa kituo cha Polisi cha kisasa kitakachokabidhiwa kwa Jeshi la Polisi, zimefikia zaidi ya shilingi bilioni moja.
- Pre GE2025 - Musukuma: Milango iko wazi kwa yeyote mwenye nia ya kugombea ubunge katika jimbo Geita Vijijini