Mbunge Musukuma: Tunafuata bidhaa Uganda zilizopita kwenye bandari yetu. Hatuoni aibu?

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Mbunge wa Geita Vijijini, Musukuma Kasheku akichangia bajeti kuu amesema Tanzania tuone aibu, haiwezekani bidhaa za Uganda zinapita bandari ya Tanzania, halafu sisi tunazifuata huko

"Leo hii sisi Watanzania tunafuata bidhaa Uganda na Kenya hamuoni aibu?, bandari inayotumika ni ya Dar es Salaam kuchukua mizigo kuipeleka Uganda halafu sisi tunaifuata Uganda kuileta Tanzania hii haiwezekani tumekosea wapi?, lazima muangalie tukiiua Kariakoo tutakuja kushikana mashati humu ndani hiyo ndiyo kila kitu kwa Tanzania lazima tupalinde,"

Musukuma.png
 
Bandani ilipokuwa inagawiwa kwa waarabu hakuliona hili? Si ndiyo wapiga chapua hawa?
 
Tatizo ni kodi utitiri na tozo nyingi za kijinga. Mbaya zaidi hata hiyo kodi inatumika kwenye anasa za viongozi wa serikali: kuzurula na wasanii nchi za nje, kununua maV8, na posho za watawala.

Umaskini wa akili ni mbaya kuliko wa aina yoyote. Viongozi ni maskini wa akili, wanawaibia ndugu zao. Wananchi nao ni maskini wa akili, licha ya kufanyiwa udhalimu mbalimbali na watawala wao, kwa uchawa wa kijinga kabisa, wanaimba mapambio ya kuwasifu watawala dhulumati.
 
Bandani ilipokuwa inagawiwa kwa waarabu hakuliona hili? Si ndiyo wapiga chapua hawa?
Alichokisema Musukuma ni tatizo la muda mrefu halikuanza juzi ni tatizo la ushuru hapa kwetu,wataalam wetu wa kodi waache kutoza kodi kubwa ikibidi wakajifunze kwa wenzetu waliofanikiwa.
Tanzania kodi ipo juu sana.
 
Kama umewahi kutumia bandari ya Dar unaweza kuelewa ni kwa nini nilisema hivyo. Ni kuwa waliacha ku-deal na tatizo hasa na wakakimbilia kugawa bandari. Ila sikupingi kuwa tuna tatizo la kodi.
 
Alichokisema Musukuma ni tatizo la muda mrefu halikuanza juzi ni tatizo la ushuru hapa kwetu,wataalam wetu wa kodi waache kutoza kodi kubwa ikibidi wakajifunze kwa wenzetu waliofanikiwa.
Tanzania kodi ipo juu sana.
Unawaita watalam wa Kodi, Hawa ni majambazi wakubwa! Wanatakiwa kunyongwa! Aliesema kama huwezi kulipa tozo hamia Burundiiiiiii? Nchi za wenzetu angejiuzulu mara Moja!
 
Back
Top Bottom