Mbunge Mwalunenge azomewa kwa Kuwataka Madereva wa Bodaboda Wachangie Sh1,000 kwaajili ujenzi wa barabara

Mbunge Mwalunenge azomewa kwa Kuwataka Madereva wa Bodaboda Wachangie Sh1,000 kwaajili ujenzi wa barabara

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
Aibu hiyo Kabambe imemkuta katika Mkutano uliohusisha Madereva wa bodaboda

Anatuhumiwa kuwasilisha bungeni hoja ya bodaboda kuchangia elfu 1 kila siku ili wajenge barabara za Mbeya

Mkutano huo uliitishwa kitapeli huku wahudhuriaji wakiamini uliitishwa na Mwenyekiti wa halmashauri, lakini kumbe ilikuwa njama ya mbunge huyo kujisafisha

UJUMBE: ALILE KHAKO
==========
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini amezomewa na madereva wa bodaboda wakati wa mkutano aliofanya leo, baada ya kutoa kauli inayowataka madereva hao pamoja na wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga kuchangia shilingi 1,000 kila mmoja kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Soma Pia: Mwalunenge: Machinga, Bodaboda siyo Maskini, wakichanga Tsh. 1,000 kila siku wanaweza hata kujenga barabara

Kauli hiyo imezua hisia tofauti miongoni mwa madereva wa bodaboda, ambao walionekana kutofurahishwa na pendekezo hilo. Katika mkutano huo, baadhi ya madereva hao walionekana wakimzomea mbunge huyo wakionyesha kutoridhishwa na kauli yake.

 
Tatizo halijawahi kuwa kuongeza kodi, hata tozo za simu ziliongezwa kipi kimefanyika zaidi ya watu kutii amri ya kula kwa urefu wa kamba ?

Barabara kilometa moja ni milioni 800, kwa siku wakiweza kukusanya kwa watu elfu 10 ni milioni 10, hio milioni 800 hadi ifike ni siku 80, imeisha yote kwenye posho za kamati ya ukusanyaji
 
"Wabunge" wenyewe wanajiteua. Kuzungumza lolote lile haliwasumbui. Hawana wajibu kwa yoyote yule kama "mwenyekiti" wao samia aliyejiapisha mafichoni.
 
Kwa utaratibu wa kuchaguliwa wabunge na serikali hata wakitaka mavi yawe mbunge wanaweza hivyo ubunge sio jambo la wananchi kwa sasa bali serikali ndiyo inaamua
Kweli kabisa. Huwa nashangaa kusikia mtu anasema eti sijui fulani 2030 harudi bungeni. Mamlaka/Rais/CCM ikimtaka mtu aingie bungeni, ataingia tu. Wananchi mtake msitake.
 
Tatizo halijawahi kuwa kuongeza kodi, hata tozo za simu ziliongezwa kipi kimefanyika zaidi ya watu kutii amri ya kula kwa urefu wa kamba ?

Barabara kilometa moja ni milioni 800, kwa siku wakiweza kukusanya kwa watu elfu 10 ni milioni 10, hio milioni 800 hadi ifike ni siku 80, imeisha yote kwenye posho za kamati ya ukusanyaji
Si mlimchagua wenyewe?
 
Back
Top Bottom