Mbunge Mzeru awapa tabasamu UWT Wilaya ya Morogoro Mjini

Mbunge Mzeru awapa tabasamu UWT Wilaya ya Morogoro Mjini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE MZERU AWAPA TABASAMU UWT WILAYA YA MOROGORO MJINI.

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro Mhe. Norah Mzeru amekabidhi Cherehani ya kudarizi yenye thamani ya shilingi 500,000 katika Uongozi wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini.

Makabidhiano hayo yamefanyika 02 Agosti, 2023 katika Ofisi ya UWT Wilaya ya Morogoro Mjini kwa lengo la kuwainua wanawake wa morogoro mjini ili waweze kuwa na mradi na kuweza kukidhi Mahitaji yao.

Mhe. Norah Mzeru amewataka wanawake kuanzisha vikundi na miradi mbalimbali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kuwaeleza kuwa endapo watapata changamoto yoyote basi wasisite kumtaarifu ili kama kuna uwezekano watasaidiana.

Vilevile, ameukabidhi Uongozi wa UWT Kata ya Lukobe, Jora la kitambaa cha CCM kwa lengo la kuendeleza mradi wao wa ushonaji huku akiwahasa waendelee kushirikiana.

Sanjari na hayo amewaomba wanawake kuunga mkono juhudi anazozifanya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuwa amekamilisha miradi mingi na nyingine anaendelea kuzitekeleza.

Naye Katibu wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, Bi. Judith Usaki, amemshukuru Mhe. Mzeru huku akimuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika utendaji wake wa kazi.

"Mbunge wetu hapa ni nyumbani, UWT Wilaya tutaendelea kukupa ushirikiano ,hiki ulichokitoa ni kikubwa sana kwetu, tunaamini fedha na vitendea kazi ulivyotupa vitakwenda kuleta mabadiliko chanya katika Jumuiya yetu ya UWT" Amesema Usaki.

 
Back
Top Bottom