Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NANCY HASSAN NYALUSI - AMEIULIZA MASWALI WIZARA YA NISHATI, BUNGENI, DODOMA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Nancy Hassan Nyalusi amemuuliza swali Waziri wa Nishati Bungeni, Dodoma leo tarehe 11 Aprili, 2023
Je, ni lini Serikali itakamilisha usambazaji wa umeme katika Vijiji 8 vya Wilaya ya Mufindi ambavyo havijapata umeme?
Akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba; Mhe. Wakili Stephen Byabato amejibu kama ifuatavyo;
"Wilaya ya Mufindi ina jumla ya Vijiji 10 tu ambavyo havina umeme ambavyo vinapatiwa umeme kupitia mradi wa kusambaza umeme Vijijini(REA) awamu ya III mzunguko wa II" - Mhe. Wakili Stephen Byabato
"Hadi kufikia Aprili 2023 Vijiji 8 vilikuwa vimeshapatiwa umeme na Vijiji 2 vijulikanavyo kama Itika na Mpangatazara bado havijapatiwa umeme. Vijiji vyote vinatarajiwa kupata umeme ifikapo mwezi Juni 2023." - Mhe. Wakili Stephen Byabato
Swali la Nyongeza;
"Ni lini Serikali itakamilisha kupeleka umeme katika Kijiji cha Idunda na Furuti, Kata ya Kimara, Wilaya ya Kilolo? - Mhe. Nancy Nyalusi
"Ni lini Serikali itaanza kusambaza Umeme katika Vitongoji Mkoani Iringa?" - Mhe. Nancy Nyalusi
"Vijiji vya Mufindi vitakamilika kupata umeme mwezi Juni 2023 kwa mujibu wa Mkataba, lakini Vijiji vingine vyote nchini kama vya Kilolo kabla ya mwezi Disemba 2023 vitakuwa vimefikishiwa umeme kwa mujibu wa mkataba kwenye REA III mzunguko wa II." - Mhe. Wakili Stephen Byabato.
"Tunaendelea na taratibu za kutafuta pesa kufikisha umeme kwenye Vitongoji vyote karibia elfu 36,000 tulivyokuwanavyo nchi nzima katika miaka minne au Mitano inayokuja kwa gharama ya shilingi Trillion 6 na Bilioni 500." - Mhe. Wakili Stephen Byabato
MaswaliNaMajibuBungeni