Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE NDAISABA RUHORO ACHANGIA 1,200,000 JUMUIYA YA WATUMIAJI MAJI - KASULO
"Nimechangia Mita 40 za kurekodi matumizi ya maji, na kiasi cha TZS 1,200,000 kama gharama ya ufundi wa kuzifunga mita hizo kwa wateja wa mwanzo" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Lengo likiwa ni kuhamasisha Wananchi kujiunga na Huduma ya maji, lakini pia kuongeza uwajibikaji na kuamsha ari ya kulipia ankara za Maji kwa wakazi wa Kasulo na Kigando" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Hiyo ni kutokana na kilio cha muda mrefu cha wananchi hao kuhitaji huduma ya maji safi na salama huku wakiwa na mradi wa maji wa zamani uliochoka na miundombinu yake kushindwa kukidhi mahitaji." - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara