Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE NDAISABA AIPA SOMO TANAPA JUU YA MADINI YALIYOPO HIFADHI YA MANYARA
"Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mzuri na kwa maono makubwa aliyonayo kwa watanzania hasa kwa kuendelea kufungua fursa kwenye kujiajiri kwenye Sekta mbalimbali za uzalishaji" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Nampongeza Waziri wa Maliasili Mhe. Mchengerwa na Utalii pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuweza kutafsiri maono ya Rais Samia. Sasa tunaona wafuga Nyuki eneo hili linaendelea kuchagizwa" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Nampongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa uongozi wako mzuri. Wananchi wa Mbeya na Watanzania wajue kuwa Watanzania tunakukubali ya kuwa na wewe unastahili Maua yako" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Naunga mkono hoja Azimio la kurekebisha mipaka; Mipaka ya Ruaha na Azimio la kushusha kwenye hifadhi ya Taifa kwenda kwenye Mamlaka ya hifadhi ya Misitu Tanzania (TFS). Azimio la kurekebisha Mipaka ndio Muarobaini wa kupeleka suluhisho la Kudumu kwa wananchi wa Ruaha" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Mataifa ya DRC, Rwanda na Burundi kwa sehemu kubwa yamekuwa yakiingiza Asali inayotoka kwenye hifadhi ya Kigosi. Wananchi wa Ngara ni watumiaji wazuri wa Asali. Asali tunayoitumia Ngara tumekuwa tukiinunua Kigosi matharani wananchi wa Kanda ya Ziwa na Mkoa wa Kagera" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Kuitoa hifadhi ya Taifa ya Kigosi na kwenda kuwa hifadhi ya Misitu kinakwenda kufungua ajira kwa watanzania zaidi ya 5,000 wanaokwenda kujiajiri moja kwa moja kwenye ufugaji wa Nyuki. Watanzania zaidi ya 10,000 wanakwenda kupata ajira kutokana na Uwekezaji wa watanzania wanaokwenda kuwekeza kufuga Nyuki" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Serikali ilikuwa na nia nzuri kupitia TFS ambapo viwanda 5 vimejengwa kwaajili ya kuchakata Asali mbichi. Kwa siku moja viwanda vilikuwa vinachakata zaidi ya Tani Nne za Asali na kwa mwaka mmoja viwanda vilikuwa vinachakata Tani 1,460 za Asali. Tani Moja ya Asali inauzwa Shilingi Milioni 4. Kwa mwaka mmoja ni takriban ni Shilingi Bilioni 5.8 za Asali" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Eneo la Kigosi baada ya kuchukuliwa na TANAPA shughuli zote za uzalishaji Asali zilisitishwa. Mwaka 2022-2023 watalii walioenda Kigosi ni Watalii 10 tu. Nchi imewekeza inawalipa watu mishahara na Mafuta kwenye magari huku tumezuia watanzania kutengeneza Shilingi Bilioni 5.8" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Ukifanya mahesabu zaidi ya Shilingi Bilioni 30 zimepotea. Dhamira nzuri ya Serikali inaonekana pale ambapo Serikali imefanya upembuzi yakinifu kwa kuangalia faida na hasara zilizopo kwenye ajira za watanzania. Nampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi mzuri kwenye hili" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"TANAPA hili la Kigosi liwe ni fundisho kwao. Hifadhi ya Manyara eneo la Mayoka lina mkondo wa Madini ambapo Madini yale hayahitaji matumizi ya Kemikali. Kipande kidogo kinauzwa dollars laki moja." - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara