Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
06/12/2024
Mbunge wa Jimbo la Ngara Mh Ndaisaba G Ruhoro kwa ushirikiano na Ofisi ya Kilimo Wilaya wameshiriki kumkabidhi mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi na umaliziaji wa soko la Kimkakati Kabanga. Hii ni utekelezaji wa ahadi ya RUHORO na DIWANI wa Kabanga Mh Hafidhi Abdallah waliyo itoa kwa wananchi wa Kabanga na Ngara mwaka 2020.
Akiongea na wananchi waliohudhuria makabidhiano hayo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutoa fedha Bilion 1.2 Tzs ili kuwezesha umaliziaji wa ujenzi wa soko hilo. Lakini pia ameowaomba wananchi waliokuwepo kuunga mkono juhudi za serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha ifikapo mwakani 2025 wakati wa uchaguzi kuipa ushindi CCM.
Mkandarasi Kitandu Infratech akiongea na wananchi waliokuwepo amewaomba kumpa ushirikiano Mh Mbunge Ndaisaba na kuhakikisha mwakani anaendelea kuwa Mbunge wao.
Aidha Mkandarasi amethibitisha kupokea fedha kiasi cha Tsh Milioni 181 ambapo amesema utekelezaji wa ujenzi utaanza tarehe 20/12/2024 na kukamilika ndani ya kipindi cha miezi Sita (6).
Soko hili lilitelekezwa tokea mwaka 2014 Ila lilianza kupata mwelekeo wa kujengwa Baada ya Mh RUHORO kulipigania ikiwemo kuliongelea Bungeni zaidi ya Mara mbili kwa nyakati tofauti tofauti.
MH RUHORO amempongeza Waziri wa Kilimo Mh Hussein BASHE kwa kuridhia na kusimamia na kuhakikisha maombi ya fedha yanapata baraka kwa ajili ya ujenzi wa soko hili la kimukakati.
Ernest RUHUGU
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Ngara