Mbunge Ndaisaba Ruhoro Ataka Vituo vya Forodha Kufanya Kazi saa 24, Ngara

Mbunge Ndaisaba Ruhoro Ataka Vituo vya Forodha Kufanya Kazi saa 24, Ngara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amemshauri Mbunge wa Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro kushirikiana na Mamlaka husika ili kuangalia uwezekano wa ujenzi wa Kituo cha Forodha cha Mugoma, mkoani Kagera baada ya kujiridhisha pasipo shaka iwapo eneo hilo linafaa kwa ujenzi wa Kituo hicho.

Dkt. Nchemba alisema hayo bungeni, jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Forodha cha Mugoma.

Alisema kuwa endapo Mamlaka husika zitajiridhisha pasipo shaka kuhusu eneo hilo kutokuwa na madhara kwa nchi kiuchumi, kijamii na kiusalama, Serikali itashauriwa kuyafanyia kazi maombi hayo.

“Kabla ya eneo au kituo kuteuliwa kuwa eneo la Forodha na kuweza kufunguliwa kama kituo cha forodha mahali popote nchini kuna taratibu za kisheria ambazo inabidi zifuatwe”, alisema Dkt. Nchemba.

Alieleza utaratibu huo kuwa ni pamoja na kutangazwa na kuchapishwa kwenye Gazeti la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, kwa mujibu wa Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ya Mwaka 2004, Kifungu Namba 11.

"Vituo viwili vya forodha vya Kabanga na Mrusagamba vinafungwa Saa Moja kamili za jioni hali inayosababisha adha ya wasafiri wa mabasi kutoendelea na safari zao na magari makubwa kusitisha kupeleka mizigo nje ya nchi. Ni upi mpango wa Serikali wa kuruhusu Vituo vya forodha viweze kufanya kazi Masaa 24 ili kuhuisha biashara ya mpakani?" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara.

Nchemba alisema kuwa baada ya Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa kupokea maombi ya kuteua eneo husika kuwa eneo la forodha kutoka kwa Waziri mwenye dhamana, huwasilisha pendekezo la kuteua kituo husika kwa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

ngara-picasdfrty.jpg
Screenshot 2024-06-11 at 23-35-26 Mange Kimambi (@mangekimambi81) • Instagram photos and videos.png
 
Back
Top Bottom