Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Jumapili ya tarehe 11 Mei 2025 alishiriki ibada katika Kanisa la Anglican Kabanga ambapo alitoa Sadaka ya Shilingi Milioni Mbili (2,000,000) ili kuunga mkono ujenzi wa Kanisa hilo.
Akisalimiana na waumini kwenye Kanisa la Anglican Kabanga, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro aliwakumbusha na kuwasisitiza wananchi kushiriki uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 kwa kuchagua viongozi wa CCM akiwemo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania na mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ameendelea kuandika rekodi ya kushirikiana na taasisi za kidini nyingi Jimboni katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku