Mbunge Ndaisaba Ruhoro: Mfanyabiashara wa soko la sukari anauza kilo moja kwa Tsh. 10,000. Hatuwezi kukubali Wananchi wetu kuteseka

Mbunge Ndaisaba Ruhoro: Mfanyabiashara wa soko la sukari anauza kilo moja kwa Tsh. 10,000. Hatuwezi kukubali Wananchi wetu kuteseka

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
"Sukari ni chakula, watanzania wa hali ya chini wanategemea Sukari kuweza kunywa Chai. Suala la Sukari ni suala la Usalama wa Nchi kwasababu chakula ni suala la kiusalama ndani ya Taifa. Hatutakiwi Kufanya Mchezo na Suala Linalogusa Usalama wa Nchi" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Suala la Sukari kwa muda mrefu tulikuwa tumeliacha kwenye mikono ya wafanyabiashara watano mpaka saba. Walikuwa wanakwenda kununua Sukari kwenye Soko la Dunia, wanachukua Sukari mwa bei ndogo wanaileta nchini wanaificha, Mtanzania wa kawaida Masikini analima Mahindi anavuna baada ya miezi mitatu anauza Kilo Moja ya Mahindi kwa Tsh. 300 lakini mfanyabiashara wa Soko la Sukari analeta Sukari ndani ya siku 28 anauza Kilo Moja kwa Tsh.10,000. Hatuwezi kukubali kuona wananchi wetu wanateseka"

"Naungana na wabunge na watanzania wote wenye mapenzi mazuri na nchi yao kuunga mkono Muswada wa Sheria ulioletwa na Mhe. Hussein Bashe hapa Bungeni kuhakikisha tunaiwezesha NFRA iweze kuingiza Sukari nchini"

"Kazi ya NFRA ni kwaajili ya kupeleka huduma kwa wananchi. Kazi ya wafanyabiashara ni kupiga faida. Wabunge tunapambana kuona wananchi wetu wanapata huduma kwa bei nafuu, wafanyabiashara wanapambana kuingiza Sukari kuificha ili kuwapiga wananchi wetu fedha nyingi "

"Mtanzania anayeuza Kilo Moja ya Maharage kwa Tsh. 600 na Kilo Moja ya Mahindi kwa Tsh. 300 hatuwezi kwenda kumuuzia Sukari kwa Tsh. 10,000. Jambo hili haliwezekani kamwe asilani" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"TEMESA wananikwaza sana, hii ni taasisi inayotakiwa kufumuliwa yote. TEMESA tumewapa kazi ya kujenga Kivuko cha Kaninya na Mayenzi mwaka 2021 lakini mwaka wanatupiga danadana, Wakandarasi wamefikisha kila kitu lakini TEMESA hawataki Kukamilisha mchakato wa kushusha kivuko ili wananchi waanze kupata huduma maeneo yale"

"Ikiwezekana TEMESA wafanyiwe ukaguzi tuangalie utendaji kazi wao, haiwezekani Kivuko cha Shilingi Milioni 100 unakijenga kwa miaka 4-5. Kivuko cha kwenda Rusumo kimeharibika hii ni wiki ya tatu wananchi hawapati huduma, TEMESA wametulia tu hawafanyi chochote"

"Wananchi wa Jimbo la Ngara tuna Barabara tuliyoahidiwa kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita na Serikali haijaanza ujenzi. Ni Barabara kutoka Mrugarama - Rulenge - Tembo Nickel - Kumbuga - Nyakahula. Serikali iliahidi kuijenga kwa kiwango cha lami"

"Wananchi wameshafanyiwa tathimini lakini fidia haijatoka. Naomba Serikali iende ikalipe fidia kwasababu wananchi wamesubiri na wamechoka. Mkandarasi ambaye ameshapatikana awezeshwe apewe fedha aanze kujenga Barabara kwa kiwango cha lami" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara



PIA SOMA
- Mbunge Ndaisaba Ruhoro Alilia Serikali Bei ya Mahindi

- Mbunge Ndaisaba Ruhoro Aililia Serikali Sakata la Kikokotoo
 
Ambao hamkuwepo ni kwamba miaka ya themanini lilikuwepo shirika la serikali la kuendeleza sukari (SUDECO), hata hivyo nalo lilikuwa linaficha sukari mpaka inayeyuka ndani ya godauni na kuwavutia nyuki! Nyerere alilivunja na kuwafukuza kazi watumishi wake, tatizo la sukari ni utamu wake tofauti na chumvi.
 
Na umri wanguu huu na ugumu wa maisha ukiwapo sijashudia tz sukari kilo ikafika elfu saba achilia elfu kumi , labda Mbunge ipo nchi ya tz nyingie anaishi
 
Back
Top Bottom