PreGE2025 Mbunge Neema Lugangira ataka Ilani ya CCM ijayo izingatie maendeleo ya kidijitali na matumizi sahihi ya AI kwa manufaa ya Taifa

PreGE2025 Mbunge Neema Lugangira ataka Ilani ya CCM ijayo izingatie maendeleo ya kidijitali na matumizi sahihi ya AI kwa manufaa ya Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Neema Lugangira, ametamani Ilani ijayo ya chama hicho izingatie kwa kina maendeleo ya kidijitali na matumizi sahihi ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence - AI) kwa manufaa ya taifa.

Akizungumza na wanahabari katika viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, Mhe. Lugangira amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Serikali kuweka mazingira rafiki kwa ukuaji wa sekta ya Asasi Zisizo za Kiserikali (NGOs), huku akitoa wito kwa jamii kuondokana na dhana potofu kwamba NGOs ni washindani wa Serikali.

Ameeleza kuwa ana matumaini Ilani ijayo ya CCM itaweka mkazo katika kuzisaidia NGOs ziweze kujitegemea na kupewa nafasi ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa, hasa ikizingatiwa changamoto ya kupungua kwa misaada ya kifedha kutoka nje kutokana na mabadiliko ya kimataifa.

 
Back
Top Bottom